VIKOMBE VIKUBWA

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Napoli 3 Chelsea 1

Jumatano, 22 Februari 2012 13:53
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_CHAMPS_LIGIMATOKEO:

Jumanne Februari 21

CSKA Moscow 1 Real Madrid 1

Napoli 3 Chelsea 1

TAARIFA:

Wakiwa huko Italia kwenye mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Chelsea, kama wenzao Arsenal ambao ndio wawakilishi wa Ligi Kuu England waliobakia kwenye michuano hiyo baada ya Man United na Man City kutupwa nje, jana walitandikwa bao 3-1 na Napoli inayocheza Serie A.

Wiki iliyopita Arsenal ilikung’utwa bao 4-0 na AC Milan.

Jana Chelsea walitangulia kupata bao katika dakika ya 17 kwa bao la Juan Mata lakini Napoli walisawazisha dakika ya 38 kwa bao la Lavezzi na kuongeza bao la pili kupitia Edinson Cavani katika dakika ya 45.

Napoli walipata bao lao la 3 dakika ya 65 na alikuwa Lavezzi aliefunga tena.

Vikosi vilivyoanza:

Napoli: De Sanctis, Campagnaro, Cannavaro, Aronica, Maggio,

Inler, Gargano, Zuniga, Hamsik, Lavezzi, Cavani.

Akiba: Rosati, Grava, Dossena, Dzemaili, Fernandez, Pandev, Britos.

Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Bosingwa, Ramires,

Meireles, Malouda, Sturridge, Drogba, Mata.

Akiba: Turnbull, Cole, Essien, Lampard, Torres, Mikel, Kalou.

Refa: Carlos Velasco Carballo [Spain]

RATIBA:

Jumatano Februari 22

[Saa 4 Dak 45 Usiku]

Basel v Bayern Munich

Marseille v Inter Milan

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90