VIKOMBE VIKUBWA

Napoli v Chelsea—Ni mechi muhimu mno kwa Chelsea!

Jumanne, 21 Februari 2012 16:22
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_CHAMPS_LIGIRATIBA:

Jumanne Februari 21

[Saa 2 Usiku]

CSKA Moscow v Real Madrid

[Saa 4 Dak 45 Usiku]

Napoli v Chelsea

Jumatano Februari 22

[Saa 4 Dak 45 Usiku]

Basel v Bayern Munich

Marseille v Inter Milan

TAARIFA:

Leo Saa 3 dakika 45, bongo taimu, Chelsea wanaingia Stadio San Paolo huko Mji wa Napoli, Italia kucheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Wenyeji wao Napoli na kwa Chelsea mechi hii ina umuhimu wa kipekee.

Kwa wengi, Meneja wa Chelsea, Andre Villas-Boas, yupo kwenye hali ngumu huku kukiwa na uvumi baadhi ya Wachezaji hawamtii hasa baada ya matokeo mabovu.

Chelsea wapo nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na wakimaliza nafasi hiyo mwishoni mwa Msimu basi hawatacheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Hivi majuzi nusura wabwagwe nje ya FA Cup baada ya kulazimika kutoa sare na Birmingham City.

Villas-Boas amekiri kuwa hajui kama bado atakuwa na kibarua ikiwa watashindwa kuifunga Napoli.

Amesema: ‘Sio juu yangu kuamua hilo, muulizeni swali hilo muhusika!’ akimaanisha aulizwe Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich.

Hata hivyo Chelsea wanakabiliana na Napoli ambayo itakuwa haina Meneja wake kwenye benchi kwa vile Meneja wao Walter Mazzarri yupo kifungoni toka kwa UEFA baada ya kutolewa nje katika mechi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI walipocheza na Villareal.

Timu zote hizi mbili huenda pia zikawakosa Wachezaji wao muhimu kwa Chelsea kumkosa Nahodha wao John Terry ambae ana maumivu ya goti na Napoli kumkosa Sentahafu wao Hugo Campanagro.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1