VIKOMBE VIKUBWA

FA CUP: Liverpool wapita kucheza Robo Fainali na Stoke City

Jumapili, 19 Februari 2012 21:32
Chapisha Toleo la kuchapisha

FA_CUP_LOGO_NEWMATOKEO:

Jumapili Februari 19

Crawley 0 Stoke 2

Stevenage 0 Tottenham 0 [Kurudiana huko White Hart Lane-tarehe kutajwa baadae]

Liverpool 6 Brighton 1

TAARIFA:

Wakiwa kwao Anfield leo Liverpool wameifunga Brighton & Hoves, Timu ya Daraja la Championship ambalo liko chini ya Ligi Kuu England, kwa bao 6-1 na kutinga Robo Fainali ya FA Cup ambako watakuwa tena nyumbani Anfield kucheza na Stoke City.

Jumapili ijayo Februari 26, Liverpool wapo Wembley kucheza Fainali ya Carling Cup dhidi ya Cardiff City, Timu nyingine ya Daraja la chini la Championship.

Kati ya bao 6 walizopata Liverpool, bao 3 ni za kujifunga wenyewe kwa mabao ya Bridcutt, bao mbili, na Dunk, na mengine yalifungwa na wenyewe Liverpool kupitia Skrtel, Caroll na Suarez ambae pia alikosa penati.

Klabu nyingine ya Ligi Kuu, Tottenham, ikicheza ugenini  na Timu ya Daraja la Ligi 1, Stevenage, ilitoka 0-0 na itabidi warudiane huko White Hart Lane ili kupata Mshindi atakaekuwa Uwanja wa nyumbani kwake kucheza na Bolton kwenye Robo Fainali.

MECHI ZA ROBO FAINALI:

Zitachezwa Wikiendi ya kuanzia Machi 7.

[Huenda zikachezwa Ijumaa, Jumamosi, Jumapili au pia Jumatatu]:

[Timu inayotajwa kwanza ipo nyumbani]

Liverpool v Stoke City

Chelsea au Birmingham v Leicester City

Tottenham au Stevenage v Bolton Wanderers

Everton v Sunderland

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90