Straika wa Chelsea Daniel Sturridge leo amefunga bao la kusawazisha kwenye mechi ya Raundi ya 5 ya FA Cup iliyochezwa Stamford Bridge dhidi ya Birmingham City iliyo Daraja la chini ya Ligi Kuu England na kumalizika bao 1-1.
Huku Washabiki wa Timu ya wageni Birmingham wakiimba ‘Utafukuzwa kazi
asubuhi!’ na huku wakiwa nyuma kwa bao 1-0 kwa bao la David Murphy la Dakika ya 20 na pia kukosa penati iliyopigwa na Juan Mata, kitanzi kilikuwa kinaonekana kuanza kumkaba Meneja wa Chelsea André Villas-Boas na hasa presha ilizidi pale pia Mashabiki wa Chelsea walipoanza pia kuzomea lakini Chipukizi Daniel Sturridge aliokoa jahazi pale aliposawazisha kwa kichwa murua katika dakika ya 62.
Mechi hii haikuonyesha kabisa picha njema kwa Chelsea inayosuasua vibaya na ambayo Jumanne inasafiri kwenda Italia kucheza na Napoli katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano wa UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Chelsea itabidi waende Uwanja wa Mtakatifu Andrew katika tarehe itakayopangwa kurudiana na Birmingham City ili kupata Mshindi atakaetinga Robo Fainali ya FA Cup
Vikosi:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel, Meireles, Sturridge, Torres, Mata. Akiba: Hilario, Essien, Lampard, Drogba, Malouda, Bosingwa, Kalou.
Birmingham: Doyle, Carr, Davies, Ibanez, Murphy, Redmond, Fahey, Mutch, Elliott, Gomis, Rooney
Akiba: Butland, Caldwell, Burke, Spector, Asante, Reilly, Jervis.
Refa: Martin Atkinson
Raundi ya 5=RATIBA/MATOKKEO:
Jumamosi Februari 18
Chelsea 1 Birmingham 1 [Kurudiana huko St Andrew Stadium. Tarehe kupangwa]
[Saa 12 Jioni]
Millwall v Bolton
Norwich v Leicester
Everton v Blackpool
[Saa 2 na robo usiku]
Sunderland v Arsenal
Jumapili Februari 19
[Saa 9 Mchana]
Crawley v Stoke
[Saa 11 Jioni]
Stevenage v Tottenham
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Liverpool v Brighton