Raundi ya 5=RATIBA
Jumamosi Februari 18
[Saa 9 na nusu mchana]
Chelsea v Birmingham
[Saa 12 Jioni]
Millwall v Bolton
Norwich v Leicester
Everton v Blackpool
[Saa 2 na robo usiku]
Sunderland v Arsenal
Jumapili Februari 19
[Saa 9 Mchana]
Crawley v Stoke
[Saa 11 Jioni]
Stevenage v Tottenham
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Liverpool v Brighton
TAARIFA:
Baada ya kufumuliwa bao 4-0 huko San Siro siku ya Jumatano na AC Milan kwenye mechi ya UEFA Championz Ligi, Jumamosi Arsenal wanatinga Stadium of Light kucheza mechi ya Raundi ya 5 ya FA Cup na Sunderland ambao Wikiendi iliyopita Arsenal waliwachapa Sunderland bao 2-1 katika mechi ya Ligi kwa bao la ushindi kufungwa dakika za mwisho na Thierry Henry ambae safari hii hatakuwepo baada ya kumaliza Mkataba wake wa mkopo.
Mbali ya mechi ya Sunderland na Arsenal pia kutakuwepo mechi nyingine 7 zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili.