VIKOMBE VIKUBWA

UEFA CHAMPIONZ LIGI: AC Milan 4 Arsenal 0

Alhamisi, 16 Februari 2012 00:53
Chapisha Toleo la kuchapisha

IBRA_v_HENRYMATOKEO:

Jumatano Februari 15

Zenit 3 Benfica 2

AC Milan 4 Arsenal 0

TAARIFA:

Ni kweli hii ni Ligi ya Mabingwa maana leo ndani ya San Siro Mabingwa wa Italia AC Milan wamewatandika Arsenal, Timu ambayo Msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England na kuingizwa kwenye michuano hii, kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Bao za AC Milan zilifungwa na Kevin Prince Boateng, Robinho, bao mbili, na Ibrahimovich kwa penati baada ya Djourou kuamua kucheza Raga badala ya Soka ndani ya boksi.

Bila shaka Arsenal watashukuru sana kufungwa bao 4 tu maana hii ilikuwa mechi ya upande mmoja na iliwachukua Arsenal dakika 66 mpaka kuweza kupiga shuti la kwanza golini kupitia Van Persie na kuokolewa na Kipa Abbiati.

Timu hizi zitarudiana Uwanjani Emirates hapo Machi 6

Vikosi:

AC Milan: Abbiati, Abate, Mexes, Thiago Silva, Antonini,

Seedorf, Van Bommel, Nocerino, Boateng, Ibrahimovic, Robinho.

Akiba: Amelia, Alexandre Pato, Nesta, Ambrosini, Bonera,

Emanuelson, El Shaarawi.

Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Song, Rosicky, Walcott, Ramsey, Arteta, van Persie.

Akiba: Fabianski, Henry, Oxlade-Chamberlain, Djourou, Arshavin, Benayoun, Coquelin.

Refa: Viktor Kassai (Hungary)

RATIBA:

Jumanne Februari 21

CSKA Moscow v Real Madrid

Napoli v Chelsea

Jumatano Februari 22

Basel v Bayern Munich

Marseille v Inter Milan

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90