VIKOMBE VIKUBWA

Wenger ategemea ushindi leo kuipa presha Chelsea!

Jumatano, 15 Februari 2012 17:46
Chapisha Toleo la kuchapisha

IBRA_v_HENRY• Bergkamp: ‘Arsenal inatabirika, haina moyo wa ushindi!’

Arsène Wenger anaamini ushindi leo kwa Timu yake Arsenal dhidi ya AC Milan huko San Siro katika mechi ya kwanza ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kufuatia ushindi kwenye FA Cup Jumamosi  watakapocheza huko Stadium of Light na Sunderland kutazidisha presha kwa Chelsea ambao wamefungana nao kwa pointi ila Arsenal wamewapiku nafasi ya 4 kwa ubora wa magoli.

Kumaliza katika nafasi 4 za juu kwenye Ligi ni muhimu mno kwani Timu hizo 4 za juu ndizo zitakazocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Wakati Wenger anajipa matumaini hayo Mchezaji wao wa zamani aliyekuwa Arsenal kwa Miaka 11 na kutwaa Ubingwa mara 3, Dennis Bergkamp, amedai kuwa Timu ya sasa ya Arsenal inatabirika na inabidi wabadilike na kuwa na moyo na ari ya ushindi badala ya kukazania mpira wa pasi nyingi tu.

Bergkamp alisema: ‘Wanacheza mchezo wa aina moja tu! Inabidi wawe na aina nyingi ya uchezaji. Pia lazima wawe na Wachezaji wengi wa kutegemewa sio kumtegemea Mchezaji mmoja ili siku akipwaya wengine wanaokoa jahazi!’

Nae Wenger amesisitiza ni muhimu kwao kufanya vizuri Wiki hii ingawa amekiri tatizo lao ni la kuwapoteza Wachezaji wao muhimu kwa kuumia na alitamka: ‘Hatuwezi kufanikiwa ikiwa kila mecha tunampoteza Mchezaji muhimu kama Per Mertesacker!’

Mertesacker huenda atakuwa nje ya uwanja kwa Msimu wote uliobakia baada ya kuumia enka.

Arsenal leo wanategemewa kumchezesha 'Mfalme' Thierry Henry kwa vile mkopo wake unamalizika na Alhamusi anatarajiwa kurudi kwenye Timu yake New York Red Bulls.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90