+++++
RATIBA:
[Mechi ni Saa 4 Dak 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Februari 14
Bayer Leverkusen v FC Barcelona
Lyon v Apoel Nicosia
Jumatano Februari 15
Zenit v Benfica [Saa 2 Usiku]
AC Milan v Arsenal
++++++
TATHMINI:
Kesho Saa 4 dakika 45 usiku, Arsenal wataingia Uwanja wa San Siro, Jijini Milan kucheza na vinara wa Serie A AC Milan katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Timu hizi zirudiana Uwanja wa Emirates hapo Machi 6.
Hali za Wachezaji:
Beki wa AC Milan Alessandro Nesta amerudi tena mazoezini baada ya kupona lakini huenda asicheze mechi hii kwa vile ni mapema kwake pamoja nae huenda Alexandre Pato akakosekana.
Mwingine ambae hatakuwepo ni Alberto Aquilani ambae bado ni majeruhi.
Arsenal wanaelekea Italy bila Sentahafu wao Per Mertesacker ambae aliumia enka kwenye mechi na Sunderland iliyochezwa majuzi lakini Fulbeki Kieran Gibbs atarudi kwenye nafasi yake kushoto na hivyo Thomas Vermaelen kucheza Sentahafu, namba ambayo ameizoea.
Majeruhi wa Arsenal ambao hawatakuweko ni Abou Diaby, Carl Jenkinson, Jack Wilshere na Andre Santos.
Straika wa Arsenal Gervinho huenda nae asicheze kwani ndio kwanza amerudi London baada ya kucheza Fainali ya AFCON 2012 hapo juzi Jumapili huko Libreville, Gabon na Nchi yake Ivory Coast iliyofungwa na Ghana.
‘Mfalme’ Thierry Henry huenda akaingizwa dakika za mwishoni kama ilivyo desturi.
Msimu uliopita:
Msimu uliopita, AC Milan na Arsenal, zote zilibwagwa kwenye hatua hii ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Arsenal kufungwa na FC Barcelona na AC Milan kubwagwa na Tottenham.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza:
AC MILAN: [Mfumo 4-3=1-2]
Abbiati, Abate, Mexes, Thiago Silva, Mesbah, Ambrosini, Van Bommel, Nocerino, Boateng, Ibrahimovich, Robinho
ARSENAL: [Mfumo 4-3-3]
Szczrsny, Sagna, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Song, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Van Persie, Walcott
RATIBA:
Jumanne Februari 21
CSKA Moscow v Real Madrid
Napoli v Chelsea
Jumatano Februari 22
Basel v Bayern Munich
Marseille v Inter Milan