VIKOMBE VIKUBWA

CHELSEA BINGWA ULAYA!

Jumapili, 20 Mei 2012 08:42
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • KOMBE• BAYERN wakosa Penati katika Dakika 30 za Nyongeza!
  • • GEMU yaamuliwa kwa Mikwaju ya Penati baada ya sare 1-1

MABAO:

Bayern Munich 1 [Muller, Dakika ya 83]

Chelsea [Drogba, Dakika ya 88]

===============

Chelsea imeibuka Klabu Bingwa ya Ulaya baada ya kuibwaga Bayern Munich Uwanja wa nyumbani kwao Allianz Arena kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Mikwaju ya Penati 4-3 hapo jana kufuatia Mechi hiyo kuwa sare 1-1 katika Dakika 90 na Dakika 30 za nyongeza kutozaa lolote.DROGBA2

Hata hivyo Bayern Munich watajililia wenyewe kwa kutotwaa Taji baada ya kutawala Mechi yote na kukosa nafasi nyingi za wazi ikiwemo penati ya Arjen Robben mwanzoni tu mwa muda wa nyongeza wa Dakika 30 ambayo iliokolewa na Kipa wa Chelsea Petr Cech.

Bila shaka Chelsea watamkumubuka sana Straika Didier Drogba ambae alisawazisha bao Dakika ya 88 na kufunga Penati ya mwisho iliyowapa ushindi.

=================

MIKWAJU YA PENATI:

Phillip Lahm (Bayern)=Afunga 1-0

Juan Mata (Chelsea)=Akosa 1-0

Mario Gomez (Bayern)=Afunga 2-0

David Luiz (Chelsea)=Afunga 2-1

Manuel Neuer (Bayern)=Afunga 3-1

Frank Lampard (Chelsea)=Afunga 3-2

Ivica Olic (Bayern)=Akosa 3-2

Ashley Cole (Chelsea)=Afunga 3-3

Bastian Schweinsteiger (Bayern)=Akosa 3-3

Didier Drogba (Chelsea)=Afunga 3-4

=================

FRANK_LAMPARDChelsea walikabidhiwa Kombe lao ambalo Nahodha John Terry, aliekuwa kifungoni, na Nahodha wa Mechi hiyo, Frank Lampard walilipokea kwa pamoja na kuamsha shamrashamra kubwa na furaha isiyo kifani iliyowaacha Mashabiki wa nyumbani wa Bayern Munich wakiwa wameduwaa na kulikumbuka pigo walilopewa na Timu nyingine ya England, Manchester United, ambao waliwatandika bao 2-1 Dakika za majeruhi kwenye Fainali ya Mwaka 1999 huko Nou Camp, Barcelona.

=================

TIMU ZA ENGLAND ZILIZOWAHI KUWA BINGWA WA ULAYA:

Liverpool (Mara 5)

Manchester United (3)

Nottingham Forest (2)

Aston Villa (1)

Chelsea (1)

=================

Mbali ya kubeba Kombe, Wadau wa Chelsea sasa watamtupia macho Mmiliki wa Klabu, Roman Abramovic, ili kujua nini hatima ya Meneja wa Muda Roberto Di Matteo na nini kitamkuta Didier Drogba, Mwenye Miaka, 34 kwani Mkataba wake ndio unamalizika.

Vikosi:

Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Tymoschuk, Contento, Schweinsteiger, Kroos, Robben, Mueller, Ribery, Gomez.

Akiba: Butt, Van Buyten, Petersen, Olic, Rafinha, Usami, Pranjic.

Chelsea: Cech, Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole, Kalou, Mikel, Lampard, Bertrand, Mata, Drogba

Akiba: Turnbull, Essien, Romeu, Torres, Malouda, Ferreira, Sturridge.

Refa: Pedro Proenca (Portugal)

 

FAINALI UEFA CHAMPIONZ LIGI: NI LEO Bayern v Chelsea

Jumamosi, 19 Mei 2012 00:00
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_CHAMPS_LIGI========================

BAYERN MUNICH v CHELSEA

-Jumamosi Mei 19,

-Saa 3 Dak 45 Usiku [Bongo Taimu]

-Uwanja: Fußball Arena München

========================

Bayern Munich leo wapo Uwanja wa nyumbani Allianz Arena, ambao kwa leo tu utaitwa Fußball Arena München, kucheza na Chelsea kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakisaka Ubingwa wao wa 5 wa Ulaya ili waungane na Liverpool kwa kuwa Timu za tatu zilizoutwaa Ubingwa huo mara nyingi nyuma ya vinara Real Madrid na AC Milan.

Chelsea wao wanasaka Ubingwa wao wa kwanza.

Kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, Chelsea na Bayern Munich zilikutana Mwaka 2004/5 kwenye Robo Fainali na Chelsea kupeta kwa jumla ya mabao 6-5 baada ya kuichapa Bayern bao 4-2 Uwanjani Stamford Bridge kwa bao za Joe Cole, Frank Lampard, bao mbili, na Didier Drogba.

Bao za Bayern zilifungwa na Bastian Schweinsteiger na Michael Ballack.

IFUATAYO ni TATHMINI ya Mechi hii:

Wachezaji watakaokosekana kwa kufungiwa:

Bayern Munich: David Alaba, Luiz Gustavo na Holger Badstuber

Chelsea: John Terry, Branislav Ivanovic, Raul Meireless na Ramires.

Vikosi vinavyoweza kuanza:

Bayern Munich (Mfumo: 4-4-1-1): Neuer; Lahm, Boateng,Tymoshchuk, Contento; Kroos, Schweinsteiger, Muller, Robben; Ribery; Gomez.

Chelsea (Mfumo: 4-3-3): Cech; Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole; Mikel, Essien, Lampard; Kalou, Mata, Drogba.

Refa: Pedro Proenca (Portugal)

USHINDANI Uwanjani:

Jerome Boateng v Didier Drogba

Baada ya kukerwa na Manchester City Msimu uliopita kwa kuchezeshwa nafasi asiyoipenda, Boateng amepewa nafasi ya Sentahafu na Bayern lakini kwenye Mechi hii atakuwa na wakati mgumu kumkabili Didier Drogba bila Madifenda wenzake wawili Holger Badstuber na Luiz Gustavo ambao wamefungiwa.

Bila shaka Drogba atatumia mwnya huo na pia kutaka kujiosha kwa kupewa Kadi Nyekundu kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2008 walipobwagwa na Manchester United.

Bastian Schweinsteiger v Frank Lampard

Hawa wote ni Wachezaji muhimu kwenye Viungo vya Timu zao na huenda wao ndio wakabadili matokeo ya Mechi hii.

Lakini kuna wasiwasi kuhusu Schweinsteiger ambae Msimu huu ameandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Kwa vile John Terry hayupo Uwanjani kwa kutumikia Kifungo, Lampard ndie atakaevaa utepe wa Unahodha.

Mario Gomez v David Luiz

Gomez, ambae amefunga bao 12 kwenye Mechi 10 za UEFA CHAMPIONZ LIGI, ndie tishio kubwa la Bayern kwa Chelsea.

David Luiz leo atasimama Sentahafu pamuja na Gary Cahill na mwenye amekiri Wiki hii amekuwa akifanya mazoezi kwenye Gemu ya PlayStation ili kupata namna ya kumkabili Mario Gomez.

TAARIFA ZA AWALI==ALHAMISI MEI 17:

========================

BAYERN MUNICH v CHELSEA

-Jumamosi Mei 19,

-Saa 3 Dak 45 Usiku [Bongo Taimu]

-Uwanja: Fußball Arena München

-REFA: Pedro Proença wa Portugal

========================

Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2011/12 itachezwa kati ya Bayern Munich na Chelsea Jumamosi Mei 19 Uwanjani Allianz Arena, ambao kwa Mechi hii tu kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München.

Wakati Chelsea na Bayern Munich zilipotinga Nusu Fainali za michuano hii wengi walidhani hawawezi kufika Fainali hasa kwa vile Wapinzani wao kwenye Nusu Fainali hizo walikuwa Vigogo wa Spain, Klabu za Real Madrid na FC Barcelona ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi.

Bayern Munich iliwabwaga Real Madrid na Chelsea ikawatupa nje FC Barcelona.

ZIFUATAZO ni DONDOO KUHUSU FAINALI HII na UKWELI NA TAKWIMU KUHUSU FAINALI ZA UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu zianze.

NJIA ILIYOWAFIKISHA FAINALI:

NJIA_ILIYOWAFIKISHA_FAINALI

UWANJA:

Allianz Arena, ambao kwa Mechi hii tu kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München.

UWANJA

Huu ni Uwanja wa nyumbani wa Timu za FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen na uliteuliwa na UEFA kuwa ndio utachezewa Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Mwaka 2011/12 Januari 2009.

Ujenzi wa Uwanja huu ulikamilika tarehe 30 Aprili 2005 na Mechi ya kwanza kuchezwa ilikuwa ni Agosti 5, 2005 kati ya Bayern Munich na VfL Borussia Monchengladbach ambayo Bayern walishinda bao 3-0 wakishuhudiwa na Watazamaji 60,000 waliojaza Viti vyote.

KOMBE:

KOMBEMachi 1967, UEFA iliamua kuiruhusu Real madrid ilichukue moja kwa moja Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kulitwaa mara 6.

Kombe jipya lina urefu wa Sentimita 62 na uzito wa Kilo 7.5 na limetengenezwa kwa Madini ya Fedha.

Siku hizi, kwa mujibu wa kanuni za UEFA, Timu inaruhusiwa kulichukua Kombe hilo moja kwa moja ikiwa tu imeshinda Ubingwa wa Ulaya kwa jumla ya mara 5 au kushinda mara Kombe hili 3 mfululizo.

Hadi leo, baada ya Miaka 50 ya Mashindano haya, ni Real Madrid CF, AFC Ajax, FC Bayern München, AC Milan na Liverpool FC pekee ambazo zimeweza kupewa Kombe hili moja kwa moja.

MPIRA:MPIRA

Mpira utakaotumika kwenye Fainali hii wa Kampuni ya Adidas unaitwa ‘Finale Munich’.

Hata hivyo, Mpira huu umekuwa ukitumika kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wote huu.

BALOZI MAALUM WA FAINALI-Paul Breitner

Paul Breitner, Miaka 60, aliwahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya akiwa na Bayern Munich, kuifungua Ujerumani bao kwenye Fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa Mjini Munich na maishani mwake amekulia Kilomita 50 tu toka Uwanja wa Allianz Arena.

Yeye ndio Balozi Maalum wa Mechi hii ambae pia aliwahi kuichezea Real Madrid.

UKWELI na TAKWIMU KUHUSU FAINALI ZA UEFA CHAMPIONZ LIGI

FAINALI=19

Ushindi=14

Sare=5

Magoli=49

Mechi kwenda Dakika 30 za nyongeza=5

Mechi kumalizwa kwa Mikwaju ya Penati=5

Matokeo ya kawaida= Bao 2-1 [Mara 4]

Timu zote mbili kufunga Mabao=Mara 10

Timu moja kufunga Mabao=Mara 8

Sare 0-0=Mara 1

Jumla ya Dakika zilizochezwa Fainali zote= 1860

Kadi Nyekundu=2

USHINDI MKUBWA

4-0     AC MILAN v FC Barcelona (Athens) 1994

3-0     REAL MADRID CF v Valencia CF (Paris) 2000

3-0     FC PORTO v AS Monaco FC (Gelsenkirchen) 2004

3-1     BV BORUSSIA DORTMUND v Juventus    (Munich) 1997

3-1     FC BARCELONA v Manchester United FC (Wembley) 2011

USHINDI MKUBWA HAFTAIMU

3-0     AC MILAN v Liverpool FC (Istanbul) 2005

2-0     AC MILAN v FC Barcelona (Athens) 1994

2-0     BV BORUSSIA DORTMUND v Juventus (Munich) 1997

FAINALI ZILIZOAMULIWA KWA PENATI

1996 JUVENTUS waliitoa AFC Ajax 4-2 baada ya sare 1-1

2001 FC BAYERN MÜNCHEN waliitoa Valencia CF 5-4 baada ya sare 1-1

2003 AC MILAN waliifunga Juventus 3-2, sare 0-0

2005 LIVERPOOL FC waliibwaga AC Milan 3-2, sare 3-3

2008 MANCHESTER UNITED FC waliitoa Chelsea FC 6-5, sare 1-1

GOLI NYINGI KUFUNGWA NA MCHEZAJI

MBILI:

Daniele MASSARO   AC MILAN 4 FC Barcelona 0 1994

Karlheinz RIEDLE    BV BORUSSIA DORTMUND 3 Juventus 1 1997

Hernán CRESPO      AC MILAN 3 Liverpool FC 3 2005

Filippo INZAGHI      AC MILAN 2 Liverpool FC 1 2007

Diego MILITO         INTE MILAN 2 FC Bayern München 0 2010

MCHEZAJI KUFUNGA FAINALI MBILI TOFAUTI

RAÚL González (Real Madrid CF)  2000 [Bao 1l], 2002 [Bao 1]

Samuel ETO’O (FC Barcelona) 2006 [Bao 1], 2009 [1]

Lionel MESSI (FC Barcelona) 2009 [1], 2011 [1]

KLABU ZA NCHI MOJA KUCHEZA FAINALI

Real Madrid CF 3 Valencia CF 0 Paris 2000

AC Milan 0 Juventus 0 Manchester         2003

[AC Milan walishinda kwa penati 3-2]

Manchester United FC 1 Chelsea FC 1 Moscow 2008

[Manchester United FC penati 6-5]

VIWANJA VILIVYOWAHI KUCHEZEWA FAINALI (Mara zake kwenye Mabano)

AMSTERDAM (1) (Amsterdam Arena, 1998)

ATHENS (2) (Olympic Stadium, 1994, 2007)

BARCELONA (1) (Camp Nou, 1999)

GELSENKIRCHEN (1) (Arena AufSchalke, 2004)

GLASGOW (1) (Hampden Park, 2002)

ISTANBUL (1) (Atatürk Olimpiyat Stadi, 2005)

LONDON (1) (New Wembley Stadium, 2011)

MADRID (1) (Estadio Santiago Bernabéu, 2010)

MANCHESTER (1) (Old Trafford, 2003)

MILAN (1)     (Stadio Giuseppe Meazza, 2001)

MOSCOW (1) (Luzhniki, 2008)

MUNICH (2) (Olympiastadion, 1993, 1997)

PARIS (2) (Stade de France, 2000, 2006)

ROME (2) (Stadio Olimpico, 1996, 2009)

VIENNA (1) (Ernst-Happel-Stadion, 1995)

WACHEZAJI WALIOKOSA FAINALI KWA KUFUNGIWA

Alessandro COSTACURTA & Franco BARESI (AC Milan) v FC Barcelona 1994

Michael REIZIGER (AFC Ajax) v Juventus 1996

Roy KEANE & Paul SCHOLES (Manchester United FC) v FC Bayern München 1999

Amedeo CARBONI (Valencia CF) v Real Madrid CF 2000

ZE ROBERTO (Bayer Leverkusen) v Real Madrid CF 2002

Pavel NEDVED (Juventus) v AC Milan 2003

Eric ABIDAL & DANIEL ALVES (FC Barcelona) v Manchester United FC 2009

Darren FLETCHER (Manchester United FC) v FC Barcelona 2009

Franck RIBÉRY (FC Bayern München) v FC Internazionale Milano 2010

THIAGO MOTTA (FC Internazionale Milano) v FC Bayern München 2010

José PINTO (FC Barcelona) v Manchester United FC 2011

KADI NYEKUNDU KWENYE FAINALI

Jens LEHMANN  ARSENAL FC v FC Barcelona [Mwaka 2006 Dakika ya 18]

Didier DROGBA CHELSEA FC v Manchester United FC [2008 Dak ya 116]

KLABU ZILIZOWAHI KUCHEZA FAINALI

Mara 6

AC Milan (1993, 1994, 1995, 2003, 2005, 2007)

Mara 4

FC Barcelona (1994, 2006, 2009, 2011), Juventus (1996, 1997, 1998, 2003), Manchester United FC (1999, 2008, 2009, 2011)

Mara 3

Real Madrid CF (1998, 2000, 2002), FC Bayern München (1999, 2001, 2010)

Mara mbili

AFC Ajax (1995, 1996), Valencia CF (2000, 2001), Liverpool FC (2005, 2007)

Mara moja

Olympique de Marseille (1993), BV Borussia Dortmund (1997), Bayer 04 Leverkusen (2002), FC Porto (2004), AS Monaco FC (2004), Arsenal FC (2006), Chelsea FC (2008), FC Internazionale Milano (2010)

WASHINDI WA UEFA CHAMPIONZ LIGI

MATAJI MATATU

AC Milan (1994, 2003, 2007), Real Madrid CF (1998, 2000, 2002), FC Barcelona (2006, 2009, 2011)

MATAJI MAWILI

Manchester United FC (1999, 2008)

TAJI MOJA

Olympique de Marseille (1993), AFC Ajax (1995), Juventus (1996), BV Borussia Dortmund (1997), FC Bayern München (2001), FC Porto (2004), Liverpool FC (2005), FC Internazionale Milano (2010)

NCHI AMBAZO KLABU ZAKE ZIMETWAA UEFA CHAMPIONZ LIGI

Mataji 6

SPAIN (1998, 2000, 2002, 2006, 2009, 2011)

Mataji 5

ITALY (1994, 1996, 2003, 2007, 2010)

Mataji 3

ENGLAND (1999, 2005, 2008)

Mataji 2:

GERMANY (1997, 2001)

Taji 1

FRANCE (1993), NETHERLANDS (1995), PORTUGAL (2004)

FAHAMU: TATHMINI kuhusu Timu za Bayern Munich na Chelsea hasusan Wachezaji na hali za Timu hizo tutazileta Ijumaa Mei 18

 

FAINALI UEFA CHAMPIONZ LIGI: Refa ni Proenca toka Ureno!

Alhamisi, 17 Mei 2012 16:48
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_CHAMPS_LIGI========================

BAYERN MUNICH v CHELSEA

-Jumamosi Mei 19,

-Saa 3 Dak 45 Usiku [Bongo Taimu]

-Uwanja: Fußball Arena München

========================

Pedro Proença wa Portugal ndie ameteuliwa kuwa Refa waREFA_PROENCAFainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya FC Bayern München and Chelsea FC itakayochezwa Jumamosi huko Munich, Ujerumani Uwanja wa Fußball Arena München.

Proenca, mwenye Miaka 41 ambae kitaaluma ni Mkurugenzi wa masuala ya Fedha, atasaidiwa na Wareno wenzake Bertino Miranda na Ricardo Santos.

Marefa Wasaidizi, watakaokuwa nyuma ya Magoli, ni Jorge Sousa na Duarte Gomes na Refa wa Akiba ni Tiago Trigo.

Msimamizi wa Marefa, au kama wanavyomwita Refa wa 4, ni Carlos Velasco Carballo wa Spain.

Proenca ameshachezesha Mechi 65 za Mashindano ya UEFA na Msimu huu amesimamia Mechi 5 za CHAMPIONZ LIGI ikiwemo ile ya Mechi ya marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kati ya Inter Milan na Olympic Marseille.

 

FAINALI UEFA CHAMPIONS LIGI: Wakilala Bayern ni pigo Germany EURO 2012!

Jumanne, 15 Mei 2012 22:21
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_CHAMPS_LIGI========================

BAYERN MUNICH v CHELSEA

-MEI 19,

-Saa 3 Dak 45 Usiku [Bongo Taimu]

-Uwanja: Fußball Arena München

========================

Ikiwa Bayern Munich watafungwa na Chelsea kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo itachezwa Jumamosi Mei 19 nyumbani kwa Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena ambao kwa siku hiyo tu, kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München, hilo litakuwa pigo kubwa kwa Germany kwa ajili ya michuano ya EURO 2012 itakayochezwa Mwezi ujao kufuatana na tathmini ya Kocha wa Germany Joachim Loew.

Bayern, ambao Wiki iliyopita walitwangwa bao 5-2 na Borussia Dortmund kwenye Fainali ya German Cup, wanawania Taji lao la 5 la Ubingwa wa Klabu Barani Ulaya na Wachezaji wao 8 watajiunga na Kambi ya Timu ya Taifa ya Germany itakayowekwa huko Italia hapo Mei 25.

Kocha Joachim Loew amesema: ‘Ikiwa Bayern watafungwa na Chelsea, kufuatia kushindwa Ubingwa na German Cup na Dortmund, basi Wachezaji wangu toka Bayern watakuwa wamekufa moyo na itabidi tuwasaidie sana!’

Wachezaji wa Bayern Munich ambao wako Timu ya Taifa ya Germany ni Kipa Manuel Neuer, Mabeki Holger Badstuber, Jerome Boateng na Philipp Lahm, Wachezaji wengine ni Bastian Schweinsteiger, Thomas Mueller, Toni Kroos na Mario Gomez

Kwenye EURO 2012, Germany wako Kundi B moja pamoja na Portugal, Denmark na Netherlands.

 

GERMAN DFB POKAL: BINGWA DORTMUND!!

Jumamosi, 12 Mei 2012 23:14
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • DORTMUND_SHANGILIA• DORTMUND 5 BAYERN 2

MABAO:

Borussia Dortmund 5 [3rd Shinji Kagawa, 41st Mats Hummels, 45th, 58th & 81st Robert Lewandowski]

Bayern Munich 2 [25th Arjen Robben, 75 Ribery]

Kwa mara ya kwanza katika historia yao ya Miaka 103, Mabingwa wa Ujerumani, Borussia Dortmund, leo wamefanikiwa kupiga Dabo, yaani kuwa Mabingwa wa Bundesliga na kutwaa Kombe la Ujerumani, DFB POKAL kwa Msimu mmoja, walipowafumua Bayern Munich bao 5-2 kwenye Fainali huku Robert Lewandowski akipiga hetitriki.

Dortmund walitwaa Ubingwa wa Bundesliga Wiki mbili zilizopita na leo wametembeza kipigo cha 5 mfululizo kwa Bayern na kutwaa Taji la pili Msimu huu.

Msimu wa Bayern Munich utakuwa wa maafa zaidi ikiwa Jumamosi ijayo, Mei 19, watashindwa kutwaa Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI watakapocheza Fainali na Chelsea, tena nyumbani kwao Mjini Munich na Uwanja wao Allianz Arena.

WASHINDI MIAKA YA HIVI KARIBUNI:

2011 FC Schalke 04

2010 Bayern München

2009 Werder Bremen

2008 Bayern München

2007 FC Nürnberg

2006 Bayern München

2005 Bayern München

2004 Werder Bremen

2003 Bayern München

2002 FC Schalke 04

2001 FC Schalke 04

2000 Bayern München

 


Page 1 of 61

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA