UWANJANI ULAYA

EUROPA LIGI: Man City yaingia Raundi ijayo

Jumatano, 22 Februari 2012 22:25
Chapisha Toleo la kuchapisha

Wakicheza kwao Uwanja wa Etihad huku wakiwa na ushindi wa bao 2-1 walioupata ugenini huko Ureno Wiki iliyopita, Manchester City leo walijihakikishia kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada ya kuishindilia FC Porto, ambao walikuwa ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hili, kwa bao 4-0.

Bao za Man City zilifungwa na Sergio Aguero, Edin Dzeko, David Silva na David Pizarro.

Katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Man City wataanza kucheza ugenini na Mshindi kati ya Legia Warszawa ya Poland au Sporting Club ya Ureno ambao wanarudiana Alhamisi huko Ureno na matokeo ya mechi yao ya kwanza yalikuwa ni 2-2.

Katika Raundi hiyo ijayo Man City watamkosa Kiungo wao muhimu Yaya Toure kufuatia kupewa kwake Kadi ya Njano kwenye Dakika ya 65 katika mechi na FC Porto, hii ikiwa Kadi yake ya pili na hivyo kufungiwa mechi moja.

Maoni 

 
0 # robinhard chrispine 2012-02-23 10:00
naweza kuwa kati ya watu wanaopata taarifa za soka kupita facebook account yangu ya robinhard chrispine naomba majiabu kutoka kwenu
Ndugu Robin,
Unachoweza kufanya ni kufungua website www.sokainbongo.com au ku-subscribe Facebook Page yetu ambayo ni https://www.facebook.com/pages/SOKA-in-Bongo/227579427269833
Reply | Reply with quote | Quote
 

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90