UWANJANI ULAYA

LIGI za ULAYA: Real 13 mbele, Dortmund yapaa, Juve iko juu!

Jumapili, 19 Februari 2012 16:41
Chapisha Toleo la kuchapisha

Huko Spain, Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao moja na kuwafanya waifunge Racing Santander bao 4-0 na kutangulia kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 13 mbele ya Mabingwa Watetezi Barcelona ambao leo wanacheza na Valencia ambao wako nafasi ya 3.

Bao hilo la Ronaldo limemfanya azidi kupaa juu kwa Ufungaji Bora na sasa ana magoli 28 kwenye Ligi akiwa mbele ya Lionel Messi kwa bao 5.

Huko Italia, Juventus waliichapa Catania bao 3-1 na kutinga tena kileleni mwa Serie A wakiwa Pointi mbili mbele ya AC Milan.

Bao za Juve zilifungwa na Andrea Pirlo, Giorgio Chiellini na Fabio Quagliarella.

Nako Ujerumani, Mabingwa Borussia Dortmund walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hertha Berlin kwa bao la Kevin Grosskreutz na kuwafanya waongoze Pointi 3 mbele ya Borussia Moenchengladbach waliowafunga Kaiserslautern bao 2-1.

Vigogo Bayern Munich  wameshika nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya vinara Borussia Dortmund baada ya kutoka sare 0-0 na Freiburg.

Ligi hizo za Ulaya zinaendelea leo.

MISIMAMO & RATIBA LIGI ZA ULAYA:

LA LIGA

MSIMAMO=Timu za juu tu:

[Kila Timu imecheza Mechi 22]

1 Real Madrid Mechi 23 Pointi 61

2 Barcelona 48

3 Valencia 40

4 RCD Espanyol Mechi 23 Pointi 33

5 Levante 32

6 Atletico de Madrid 31

7 Malaga 31

8 Osasuna Mechi 23 Pointi 31

9 Athletic de Bilbao 30

10 Sevilla Mechi 23 Pointi 29

++++++

SERIE A

MSIMAMO=Timu za juu tu:

[Kila Timu imecheza Mechi 23 isipokuwa inapotajwa]

1 Juventus Pointi 49

2 AC Milan 47

3 Lazio 42

4 Udinese 41

5 Napoli Mechi 24 Pointi 37

6 Inter Milan Mech 24 Pointi 35

7 AS Roma 35

8 Palermo 31

9 Cagliari 30

10 Genoa 30

++++++

BUNDESLIGA

MSIMAMO=Timu za juu tu:

[Kila Timu imecheza Mechi 22 isipokuwa inapotajwa]

1 Borussia Dortmund Pointi 49

2 Borussia Monchengladbach 46

3 Bayern Munich 45

4 Schalke Mechi 21 Pointi 41

5 Werder Bremen 36

6 Bayer Leverkusen 34

7 Hannover Mechi 21 Pointi 31

8 Wolfsburg Mechi 21 Pointi 27

9 Stuttgart Mechi 21 Pointi 26

10 Hoffenheim 26

++++++

RATIBA/MATOKEO:

Ijumaa Februari 17

SERIE A

Forentina 0 Napoli 3

Inter Milan 0 Bologna 3

BUNDESLIGA

Hoffenheim 1 Mainz 1

Jumamosi Februari 18

LA LIGA

Getafe 1 Espanyol 1

Real Madrid 4 Real Racing Santander 0

Sevilla 2 Osasuna 0

SERIE A

Juventus 3 Catania 1

BUNDESLIGA

Kaiserslautern 1 Borussia Monchengladbach 2

Nuremberg 2 Cologne 1

Bayer Leverkusen 4 Augsburg 1

Hamburger 1 Werder Bremen 3

Hertha Berlin 0 Borussia Dortmund 1

Freiburg 0 Bayern Munich 0

Jumapili Februari 19

LA LIGA

Granada v Real Sociedad

Athletic Bilbao v Malaga

Real Mallorca v Villareal

Sporting Gijon v Atletico Madrid

Levante v Rayo Vallecano

Barcelona v Valencia

SERIE A

Lecce v Sienna

AS Roma v Parma

Genoa v Chievo

Cesena v AC Milan

Novara v Atalanta

Udinese v Cagliari

Palermo v Lazio

BUNDESLIGA

Schalke v Wolfsburg

Hannover v Stuttgart

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA