Inter Milan wamepata kipigo kingine cha nyumbani kwenye Serie A baada ya kutandikwa bao 3-0 hapo jana toka kwa Bologna hiki kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwao baada ya Wikiendi iliyopita kutunguliwa bao 1-0 pia wakiwa nyumbani na Timu ya mkiani Novara na haya matokeo yamezidisha presha kubwa kwa Meneja Claudio Ranieri huku Mashabiki wakililia Jose Mourinho arudishwe.
Bao za Bologna zilifungwa na Marco Di Vaio, bao mbili, na Acquafresca.
Nao Napoli, wakiwa ugenini, walijipasha kwa ajili ya mechi yao na Chelsea ya UEFA CHAMPIONZ LIGI hapo Jumanne kwa kuibonda Fiorentina bao 3-0 hapo jana.
Mabao ya Napoli yalifungwa na Edinson Cavani, bao mbili, na Ezequeil Lavezzi.
BUNDESLIGA: Hoffenheim 1 Mainz 1
Wakiwa chini ya Kocha mpya, Markus Babbel, Hoffenheim walitoka sare bao 1-1 na Mainz katika mechi pekee ya Bundesliga iliyochezwa jana.
Hoffenheim walitangulia kupata bao baada ya Nikolce Noveski kujifunga mwenyewe katika dakika ya 9 lakini Mchezaji toka Misri Mohamed Zidan alisawazisha kwa Mainz katika dakika ya 29.
MISIMAMO & RATIBA LIGI ZA ULAYA:
LA LIGA
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 22]
1 Real Madrid Pointi 58
2 Barcelona 48
3 Valencia 40
4 Levante 32
5 RCD Espanyol 32
6 Atletico de Madrid 31
7 Malaga 31
8 Osasuna 31
9 Athletic de Bilbao 30
10 Rayo Vallecano 28
++++++
SERIE A
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 23 isipokuwa inapotajwa]
1 AC Milan Pointi 47
2 Juventus Mechi 22 Pointi 46
3 Lazio 42
4 Udinese 41
5 Napoli Mechi 24 Pointi 37
6 Inter Milan Mech 24 Pointi 35
7 AS Roma 35
8 Palermo 31
9 Cagliari 30
10 Genoa 30
++++++
BUNDESLIGA
MSIMAMO=Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 21 isipokuwa inapotajwa]
1 Borussia Dortmund Pointi 46
2 Bayern Munich 44
3 Borussia Monchengladbach 43
4 Schalke 41
5 Werder Bremen 33
6 Bayer Leverkusen 31
7 Hannover 31
8 Wolfsburg 27
9 Stuttgart 26
10 Hoffenheim Mechi 22 Pointi 26
++++++
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 17
SERIE A
Forentina 0 Napoli 3
Inter Milan 0 Bologna 3
BUNDESLIGA
Hoffenheim 1 Mainz 1
Jumamosi Februari 18
LA LIGA
Getafe v Espanyol
Real Madrid v Real Racing Santander
Sevilla v Osasuna
SERIE A
Juventus v Catania
BUNDESLIGA
Kaiserslautern v Borussia Monchengladbach
Nuremberg v Cologne
Bayer Leverkusen v Augsburg
Hamburger v Werder Bremen
Hertha Berlin v Borussia Dortmund
Freiburg v Bayern Munich
Jumapili Februari 19
LA LIGA
Granada v Real Sociedad
Athletic Bilbao v Malaga
Real Mallorca v Villareal
Sporting Gijon v Atletico Madrid
Levante v Rayo Vallecano
Barcelona v Valencia
SERIE A
Lecce v Sienna
AS Roma v Parma
Genoa v Chievo
Cesena v AC Milan
Novara v Atalanta
Udinese v Cagliari
Palermo v Lazio
BUNDESLIGA
Schalke v Wolfsburg
Hannover v Stuttgart