UWANJANI ULAYA

Rangers yapokonywa Pointi 10

Jumatano, 15 Februari 2012 18:19
Chapisha Toleo la kuchapisha

Vigogo wa Soka huko Scotland, Glasgow Rangers, wamenyang’anywa Pointi 10 za Ligi Kuu Scotland baada ya kuwekwa chini ya usimamizi maalum ili kukwepa Klabu kutangazwa mufilisi kwa sababu ya madeni makubwa.

Sheria za Soka zinatamka kuwa Klabu ikiwekwa chini ya Msimamizi maalum ili kukwepa kufilisiwa hunyang’anywa pointi na ile inayotangaza imefilisika basi hufutiwa Leseni yao na FA.

Rangers, ambao ndio Mabingwa watetezi huko Scotland, wako nafasi ya pili nyuma ya Celtic kwa pointi 4 lakini kuporwa huku pointi 10 kutawafanya wawe pointi 14 nyuma ya Celtic lakini bado watashikilia nafasi ya pili.

++++++

MSIMAMO:

-Celtic Pointi 65

-Rangers 51

-Motherwell 42

++++++

Mkasa huu wa Rangers umekuja baada ya kudaiwa Pauni Milioni 78 na Idara ya Kodi ambayo imedai uongozi wa Rangers ulitumia ujanja na mbinu ili kukwepa kulipa Kodi halali kwa kuweka Mikataba feki kwa Wachezaji.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90