UWANJANI ULAYA

Ronaldinho yumo Brazil v Bosnia Februari 28

Jumanne, 14 Februari 2012 19:26
Chapisha Toleo la kuchapisha

Kikosi cha Wachezaji 23 cha Brazil ambacho kitacheza mechi ya kirafiki na Bosnia huko St Gallen, Uswisi hapo Februari 28 kimetajwa na yumo Gwiji Ronaldinho lakini Mastaa Kaka na Robinho hawamo kwenye Timu hiyo.

Ronaldinho, Miaka 31, ambae sasa ni Nahodha wa Klabu ya Flamengo huko Brazil, pia alichukuliwa kwenye Timu ya Brazil na Kocha Mano Menezes Mwezi Septemba Mwaka jana walipocheza na kuzifunga Gabon na Misri kwa bao 2-0 kila mmoja baada ya kuachwa kwa muda mrefu.

Hadi kufikia Juni Mwaka huu Brazil wanatarajiwa kucheza mechi za kirafiki na Denmark, USA, Mexico na Argentina ikiwa ni maandalizi yao kwa ajili ya Mashindano makubwa yatakayochezwa Nchini kwao ya Kombe la Mabara hapo 2013 na Fainali za Kombe la Dunia 2014.

KIKOSI KAMILI:

Makipa: Julio Cesar (Inter Milan), Diego Alves (Valencia), Rafael (Santos)

Mabeki: Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves, Adriano (both Barcelona), Alex Sandro (Porto), Thiago Silva (AC Milan), David Luiz (Chelsea), Luisao (Benfica), Dede (Vasco da Gama)

Viungo: Danilo (Porto), Elias (Sporting), Fernandinho (Shakhtar Donetsk), Hernanes (Lazio), Sandro (Tottenham Hotspur), Paulo Henrique Ganso (Santos), Lucas (Sao Paulo), Ronaldinho (Flamengo)

Mafowadi: Neymar (Santos), Leandro Damiao (Internacional), Jonas (Valencia), Hulk (Porto)

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90