UWANJANI ULAYA

LA LIGA: Real ipo Pointi 10 juu kileleni!

Jumatatu, 13 Februari 2012 09:51
Chapisha Toleo la kuchapisha

Real Madrid wamefungua pengo la Pointi 10 mbele ya Mahasimu wao FC Barcelona na kujikita kileleni mwa La Liga baada ya kuwatwanga Levante bao 4-2 hapo jana Uwanjani Bernabeu huku Cristiano Ronaldo akipiga hetitriki hiyo ikiwa hetitriki yake ya 6 kwa Msimu huu.

Levante walitangulia kufunga lakini Ronaldo akasawazisha kwa penati na kuanzia hapo njia ikafunga na kuwafanya Levante waweweseke na pia kupata pigo baada ya Mchezaji wao Vicente iborra de la Fuente kupewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 43.

Bao jingine la Real lilifungwa na Karim Benzema.

Juzi Barcelona walichapwa 3-2 na Osasuna.

Huu ni ushindi wa 7 mfululizo kwa Real kwenye Ligi tangu wafungwe 3-1 na Barca Mwezi Desemba  na umewafanya wawe nambari wani na wana Pointi 58 kwa Mechi 22 wakifuatiwa na Barca wenye Pointi 48, Valencia wapo nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 40 na wanafuata Levante na Espanyol wenye Pointi 32 kila mmoja.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1