UWANJANI ULAYA

Real Klabu Tajiri Miaka 7 mfululizo!

Alhamisi, 09 Februari 2012 16:51
Chapisha Toleo la kuchapisha

Real Madrid bado inaongoza kwa kuwa Klabu yenye kipato kikubwa Duniani ikiwa sasa ni Miaka 7 mfululizo ikifuatiwa na Mahasimu wao Barcelona na wa tatu ni Manchester United ambao ndio wanashikilia rekodi ya kuwa juu kama Klabu Tajiri kwa Miaka minane mfululizo.

Listi hiyo ya utajiri imetolewa na Kampuni ya Mahesabu, Deloitte, ambayo ni kubwa na inaheshimika katika medani hiyo na ambayo imetathmini mapato ya kila Klabu kwa Mwaka wa Fedha wa 2010/11.

Klabu zinazofuatia kwenye Listi hiyo ni Bayern Munich, Arsenal na Chelsea.

Liverpool imeporomoka nafasi moja na sasa ni wa 9.

LIGI YA UTAJIRI:

1. Real Madrid: 479.5m euros

2. Barcelona: 450.7m euros

3. Man Utd: 367m euros

4. Bayern Munich: 321.4m euros

5. Arsenal: 251.1m euros

6. Chelsea: 249.8m euros

7. AC Milan: 235.1.m euros

8. Internationale: 211.4m euros

9. Liverpool: 203.3m euros

10. Schalke: 202.4m euros

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1