UWANJANI ULAYA

Mourinho: ‘Wachezaji wanaamini hatuwezi kushinda Nou Camp!’

Alhamisi, 26 Januari 2012 18:35
Chapisha Toleo la kuchapisha

EL_CLASICO_PART_1Jose Mourinho amedai kuwa baadhi ya Wachezaji wake wa Real Madrid wana imani kuwa hawawezi kushinda Nou Camp licha ya jana kutoka nyuma kwa bao 2-0 na kumaliza mechi wakiwa 2-2 na Barcelona lakini wakatolewa nje ya Copa del Rey kwa vile walifungwa mechi ya kwanza 2-1.

Licha ya kutawala kipindi cha kwanza, Real walijikuta wakipigwa bao mbili katika dakika ya 43 na Pedro na ya 45 na Daniel Alves lakini wakasawazisha kwa bao za Ronaldo, dakika ya 68 na Karim Benzema dakika ya 72.

Imani hiyo kutokuweza kushinda Nou Camp ya Wachezaji wa Real imekuja baada ya Refa wa pambano lao la jana kuwapa Wachezaji wa Real Kadi za Njano 8 mbili zikiwa kwa Sergio Ramos alietolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Mourinho alihoji ikiwa Timu ngeni zinapocheza Nou Camp nyumbani kwa Barcelona kama zinatendewa haki na Marefa na aliongeza: ‘Nimecheza hapa na Chelsea, Inter Milan na Real na hili si jipya! Nitawapa hongera Barca kwa kile walichofanya Bernabeu Wiki iliyopita lakini si kwa mechi hii au kwenda Nusu Fainali.’

Nae Meneja wa Barcelona, Pep Guardiola, hakutaka kujiingiza kwenye ubishi huo ila alisema ameshukuru kuingia Nusu Fainali ya Copa del Rey.

Guardiola pia alitamka: ‘Real ni Timu ngumu na ushindi huu ni pongezi kwetu. Sasa ni vigumu kuifunga Real kupita ilivyokuwa na kufuzu huku kumetufanya tuwe na furaha!’

Maoni 

 
0 # Davie Wamara 2012-01-26 20:54
naipenda sana Barcelona lakini ktk mchezo wa jana ilibebwa dhahili
Reply | Reply with quote | Quote
 
 
0 # Dotto Benedict 2012-01-29 10:41
Mimi ni mpenzi wa Real Madrid, lakini tukiangalia hali halisi ya soka la sasa duniani Barcelona ni timu nzuri sana na hanastaili kabisa kwa matokeo anayo yapata uwanjani.Lakini pia naamini Madrid ni timu nzuri pia duniani lakini inabidi waondoe fikra za kuwa Barca anabebwa pia waondoe fikra kuwa hawawezi kuwafunga Barca,Wanachota kiwa wakiwa uwanjani watulize vichwa vyao na wacheze soka kama wanavyo elekezwa naamini everything is possible and they can do somthing.Ni hayo go Madrid.
Reply | Reply with quote | Quote
 

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1