Beki wa Real Madrid Pepe atacheza kwenye mechi ya marudiano ya Copa del Rey itakayochezwa Jumatano Uwanjani Nou Camp ikiwa yuko fiti licha ya kuzua mgogoro mkubwa baada ya kumkanyaga mkononi Lionel Messi katika mechi ya kwanza ya Kombe hilo iliyochezwa Wiki iliyopita huko Santiago Bernabeu na Real kuchapwa 2-1 na Barca.
Refa katika mechi hiyo ambayo Pepe alimkanyaga Messi hakuona tukio hilo na wengi walitegemea Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, litamwadhibu Mreno huyo lakini jana waliamua kutomchukulia hatua yeyote.
Pepe hakuwemo kwenye Kikosi cha Real kilichoifunga Atletic Bilbao bao 4-1 majuzi Jumapili lakini leo Kocha wa Real Jose Mourinho amethibitisha ikiwa Pepe, ambae ameumia pamoja na Viungo Lassana Diarra na Esteban Granero, watakuwa fiti atawachezesha.
Mourinho, akiongea na Wanahabari hivi leo, alikwepa kujibu maswali yaliyohusiana na mbinu atakazotumia ili kuifunga Barca Timu ambayo imemfunga mara 5 kati ya 9 alizocheza nao tangu atue Real na kuambulia kushinda mara moja tu kwa bao 1-0 alilofunga Cristiano Ronaldo kwenye Fainali ya Copa del Rey Msimu uliopita walipotwaa Kombe hilo.

![]() |