UWANJANI ULAYA

Licha ya ushindi, Mourinho azomewa!

Jumatatu, 23 Januari 2012 10:27
Chapisha Toleo la kuchapisha

jose_mourinho15Mashabiki wa Real Madrid jana walimzomea Meneja wao Jose Mourinho licha ya Timu yake kuifunga Athletic Bilbao bao 4-1 na kujizatiti kileleni mwa La Liga wakiwa pointi 5 mbele ya Barcelona ambao pia waliichabanga Malaga 4-1.

Katika mechi hiyo ya jana Cristiano Ronaldo alipachika bao mbili kwa penati.

Mashabiki wa Real walianza kuonyesha kuchoshwa na Mourinho tangu Jumatano iliyopita na kuanza kumzomea walipofungwa na Barca 2-1 kwenye mechi ya kwanza ya Copa del Rey Uwanjani Bernabeu lakini hilo halikumsitua Kocha huyo anaejiita ‘Mtu Spesheli’.

Barca na Real zitarudiana Jumatano hii huko Nou Camp katika mechi ya pili ya Robo Fainali ya Copa del Rey.

Mourinho alitamka: ‘Zidane alizomewa hapa. Ronaldo amezomewa hapa. Cristiano Ronaldo, Mshindi wa Ballon d’Or, anazomewa hapa. Kwa nini nisizomewe? Zidane aliibu hayo kwa soka lake, Ronaldo hivyo hivyo. Cristiano nae anaendelea kutandaza soka safi, mimi naendelea na kazi yangu!’

Mourinho alipokewa hapo Real kama shujaa Mwaka 2010 baada ya kuiongoza Inter Milan kutwaa Ubingwa wa Ulaya na mwenyewe amejigamba angesituka tu kama angezomewa kwenye Klabu ambayo hawana tabia hiyo.

Mourinho aliongeza: ‘Ingetokea ambako hawazomei, ningekuwa na wasiwasi lakini hapa wanazomea hata majina makubwa kwenye soka, hilo si tatizo. Haikunitokea nilipokuwa Porto, au Chelsea au Inter. Kuna mwanzo kwa kila kitu!’

Pia kuna habari zilizotangazwa na Gazeti maarufu huko Madrid, Marca, kuwa kuna msuguano kati ya Wachezaji wa Kihispania na wenzao toka nje baada ya hao wa Spain kumlalamikia Mourinho kitu ambacho kiliwakera Wachezaji toka nje.

Mourinho alikataa kuzungumzia hilo.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1