UWANJANI ULAYA

BUNDESLIGA yatoka likizo, Bayern Munich yabondwa!

Jumamosi, 21 Januari 2012 01:26
Chapisha Toleo la kuchapisha

BAYERN_SHANGILIABorrusia Monchengladbach imewachapa Bayern Munich bao 3-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Ujerumani Bundesliga baada ya mapumziko ya Majira ya Baridi yaliyoanza kabla ya Krismasi na kuthibitisha ubabe wao juu ya Wakongwe hao kwani pia waliwafunga Bayern Munich bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi siku ya ufunguzi wa Msimu huu.

Marco Reus ndie aliewapatia Borrusia Monchengladbach bao la kwanza baada ya kosa la Kipa Manuel Neuer na bao la pili lifungwa na Patrick Herrman.

Borrusia Monchengladbach waliongeza bao la 3 dakika ya 71 mfungaji akiwa tena Patrick Herrman na bao pekee la Bayern lilifungwa na Bastian Schweinsteiger dakika ya 76.

Ushindi huo umewafanya Moenchengladbach wawe nafasi ya pili wakiwa pointi moja nyuma ya Bayern lakini Schalke, ambao wanacheza na Stuttgart Jumapili, na Mabingwa Borussia Dortmund ambao wako ugenini kucheza na Hamburg, wanaweza kuwa pointi sawa na Bayern Munich ikiwa watashinda.

Maoni 

 
+1 # David chicharito 2012-01-21 07:51
Kweli kifo cha nyani miti yote uteleza
Reply | Reply with quote | Quote
 

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1