UWANJANI ULAYA

COPA del REY: Real 1 Barca 2

Alhamisi, 19 Januari 2012 02:04
Chapisha Toleo la kuchapisha

EL_CLASICO_PART_1Katika mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Copa del Rey iliyochezwa Santiago Bernabeu, Mabingwa watetezi Real Madrid walianza vibaya kwao baada ya kuchapwa bao 2-1 na Mahasimu wao wakubwa FC Barcelona.

Timu hizi zitarudiana tena Jumatano Januari 25 ijayo huko Nou Camp.

Real walianza vyema kwa kupata bao Dakika ya 11 baada ya pande zuri la Karim Benzema kumfikia Cristiano Ronaldo aliecheza vyema na kufunga bao tamu lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha Pili Barcelona walisawazisha baada ya kona kumkuta Nahodha Puyol aliefunga kwa kichwa.

Dakika ya 77 pande tamu la Lionel Messi lilimkuta Abidal alieweka gambani na kushusha na kupachika bao la ushindi.

Kwa Wadau wa Soka wasiokuwa na ushabiki wa upande wowote hii haikuwa mechi ya kuvutia kwani ilijaa vituko, udanganyifu na visasi vya chini kwa chini.

VIKOSI:

Real Madrid: Casillas; Altintop, Ramos, Carvalho, Coentrao; Lassana Diarra, Xabi, Pepe; Ronaldo, Higuaín, Benzema

Akiba: Adan, Marcelo, Albiol, Kaka, Ozil, Granero, Callejon.

Barcelona: Pinto; Dani Alves, Piqué, Puyol, Abidal; Busquets, Xavi, Iniesta; Alexis, Fábregas, Messi.

Akiba: Valdes, Mascherano, Thiago, Adriano, Sergi Roberto, Dos Santos, Cuenca

Robo Fainali:

RATIBA/MATOKEO Mechi za Kwanza

Jumanne Januari 17

Espanyol 3 Mirandes 2

Jumatano Januari 18

Athletic de Bilbao 2 Real Mallorca 0

Real Madrid 2 FC Barcelona 2

Alhamisi Januari 19

Valencia v Levante

Nusu Fainali

Real/Barca v Valencia/Levante

Espanyol/Mirandes v Athletic Bilbao/Real Mallorca

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1