UWANJANI ULAYA

COPA del REY=El Clasico: Jumatano Real v Barca

Jumanne, 17 Januari 2012 18:55
Chapisha Toleo la kuchapisha

EL_CLASICO_PART_1‘Mtu Spesheli’, Jose Mourinho ana kibarua kigumu kuhakikisha Wachezaji wake wa Real Madrid wanaingia Uwanjani kwao Santiago Bernabeu Jumatano usiku na moyo wa ushindi watakapokutana na Mahasimu wao wakubwa FC Barcelona katika mechi ya kwanza ya Robo Fainali kugombea Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain.

Mechi kati ya Real Madrid na FC Barcelona huko Spain hubatizwa jina la ‘El Clasico’.

Real wanaingia kwenye mechi El Clasico hii wakiwa wameshinda mechi 22 kati ya mechi zao zote 23 walizocheza mwisho wakiwa wamefungwa mechi moja tu ambayo ni kipigo cha bao 3-1 Wiki 6 zilizopita walichopokea toka kwa Barca kwenye mechi ya La Liga.

Tangu atwae himaya hapo Real Miaka miwili iliyopita Jose Mourinho ameweza kuifunga Barca mara moja kati ya mara 8 walizocheza na ushindi huo ni ule wa bao 1-0 alilofunga Cristiano Ronaldo katika muda wa nyongeza wa Fainali ya Copa del Rey Msimu uliopita.

Matokeo mengine katika mechi hizo 8 za El Clasico ni vipigo vinne kwa Real na sare 3.

Akiongelea mechi hii, Kiungo wa Barca, Xavi, alisema: ‘Waulize Wachezaji wa Real kama tumewapotezea ari yao. Ushindi au kufungwa kunaathiri ari na fikra za Timu. Mshindi kwenye mechi hii anapata morali kubwa.’

Siku hizi, Wadau wengi huchukulia mechi ya El Clasico kama pia ni vita binafsi kati ya Mastaa Cristiano Ronaldo wa Real na Lionel Messi wa Barca, ambae majuzi tu ametwaa Tuzo ya 3 mfululizo ya Mchezaji Bora Duniani, Tuzo ambayo aliirithi toka kwa Ronaldo alipoinyakua Mwaka 2008.

Wakati Ronaldo amefunga bao 3 tu katika El Clasico 10 zilizopita, Messi amepachika bao 7 katika mechi hizo.

Hata hivyo, Msimu huu Ronaldo ndie anaongoza katika La Liga kwa kufunga mabao 21 ukilinganisha na Messi ambae ana bao 19.

Kila Timu itawakosa baadhi ya Wachezaji wake wakati Kikosi cha Real chini ya Kocha Mourinho huenda kikamkosa Beki Pepe ambae ana maumivu lakini wanaweza kumchezesha Winga Angel Di Maria ambae amepata nafuu huku Kocha Pep Guardiola wa Barca atakuwa na Kikosi chake bila ya majeruhi David Villa, Ibrahim Afellay na Pedro wakati Seydou Keita yuko Afrika kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Robo Fainali Copa del Rey:

RATIBA Mechi za Kwanza

Jumanne Januari 17

Espanyol v Mirandes

Jumatano Januari 18

Athletic de Bilbao v Real Mallorca

Real Madrid v FC Barcelona

Alhamisi Januari 19

Valencia v Levante

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1