Tujikumbushe

Lipende au Lichukie, Vuvuzela Daima!!!

Alhamisi, 14 Julai 2011 21:17
Chapisha Toleo la kuchapisha

Lipende au Lichukie, Vuvuzela Daima!!!
Vuvuzela safarini Mtoni!!!

[Habari hii imenyotolewa toka kwenye Blogu yetu anzilishi www.uksokainbongo.blogspot.com]

vuvuzela_daimaUsishangae Msimu ujao wa Ligi Kuu England utakaoanza Agosti 14 ukianza kuziona Vuvuzela za Rangi nyekundu zikiwa Old Trafford, za rangi ya bluu zikiwa Stamford Bridge, nyeusi na nyeupe zikiwa St James Park na za rangi ya Ze Gunners zikiwa Emirates kwani Waandaaji wa Kombe la Dunia huko Afrika Kusini wamewahimiza Washabiki toka kila kona ya Dunia waliopo Afrika Kusini kushuhudia Kombe la Dunia kuzinunua Vuvuzela za rangi za Klabu zao wanazoshabikia, kuingia nazo Viwanjani huko Bondeni na kuzipuliza watakavyo na Kombe la Dunia likiisha waende na Vuvuzela zao kuzipuliza kwenye Viwanja vya Klabu zao.
Kauli hiyo ya Waandaaji hao imekuja kufuatia baadhi ya Wadau, na hasa Watangazaji na baadhi ya Timu, kudai zinaleta usumbufu na huwafanya kupoteza malengo Uwanjani na hivyo Vuvuzela zipigwe marufuku kwenye Kombe la Dunia.
Malalamiko hayo yalimfanya Danny Jordaan, Mkuu wa Kamati ya Maandalizi, kuwataka Washabiki wawe wanaimba badala ya kuzipuliza Vuvuzela mfululizo.
Nae Msemaji wa Ligi Kuu England amesema wao hawana pingamizi Vuvuzela kuvamia huko kwa sababu hamna kanuni inayopinga hilo na ni juu ya Wasimamizi wa Viwanja binafsi kuamua kama hawazitaki.
Hivi sasa kuna mjadala mkubwa unaendelea huko Bondeni huku Kombe la Dunia likiendelea kuhusu Vuvuzela lakini Waandaaji wameng’ang’ania Vuvuzela ni sehemu ya utamaduni wa Soka huko Afrika Kusini na chimbuko lake ni sehemu ya Historia yao kwani Vuvuzela zilitumika wakati wa jadi kupigisha mbiu za mgambo.
Mmoja wa Waandaaji alisema: “Hivi sasa Vuvuzela si zana ya Afrika Kusini pekee! Wageni waliopo wamezinunua kwa wingi na wataondoka nazo mara baada ya Mashindano na bila shaka utaziona Old Trafford, Stamford Bridge, Emirates, Anfield, Nou Camp, Santiago Bernabeau na huko Munich kwa Bayern!!”
Lakini kuna baadhi ya Raia wa Afrika Kusini wamedai kuna ‘Washamba’ wa Vuvuzela ndio wanaharibu matumizi yake kwani hulipuliza bila taimingi kwani wenyewe huko Bondeni hulizibua kwa pamoja Uwanja mzima pale tu kuna tukio kubwa.
Nae Msemaje wa Waandaaji alimalizia: “Mashindano haya Wenyeji ni Afrika Kusini. Nyinyi kama Wageni wetu lazima mkumbatie utamaduni wetu na jinsi tunavyoshangilia. Tufunge mjadala huu ulioendelea Mwaka mzima tangu Mashindano ya Kombe la Mabara! Ama lipende Vuvuzela au lichukie tu! Sisi Afrka Kusini tunalipenda!”

 

LIGI YA NANI ALICHUKUA UBINGWA MARA YA MWISHO

Jumamosi, 26 Februari 2011 15:18
Chapisha Toleo la kuchapisha

premier_league

[MIAKA ILIOPITA TANGU KLABU INYAKUE UBINGWA KWA MARA YA MWISHO]

MSIMAMO:

1 Chelsea, Mwaka 1 uliopita

2 Manchester United, Miaka 2

3 Arsenal, Miaka 7

4 Leeds United, Miaka 19

5 Liverpool, Miaka 21

6 Everton, Miaka 24

7 Aston Villa, Miaka 30

8 Nottingham Forest, Miaka 33

9 Derby County, Miaka 36

10 Manchester City, Miaka 43

11 Ipswich Town, Miaka 49

12 Tottenham Hotspur, Miaka 50

13 Burnley, Miaka 51

14 Wolverhampton Wanderers, Miaka 52

15 Portsmouth, Miaka 61

16 Sunderland, Miaka 68

17 Sheffield Wednesday, Miaka 74

18 Newcastle United, Miaka 77

19 Huddersfield Town, Miaka 78

20 West Bromwich Albion, Miaka 83

 

 


Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1