Manchester United v Ajax Amsterdam [Matokeo Mechi ya kwanza 2-0]
UWANJA: Old Trafford
SAA: 5 Dakika 5 Usiku
TAARIFA:
Manchester United Alhamisi usiku wanaikaribisha Ajax Amsterdam ya Uholanzi Uwanjani Old Trafford katika mechi ya marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI baada ya kuifunga Ajax bao 2-0 huko Amsterdam ArenA Wiki iliyopita.
Mshindi wa mechi hii atapambana na Mshindi wa Mechi kati ya Athletic Bilbao na Lokomotiv Moscow kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na matokeo ya mechi ya Timu hizi katika mechi yao ya kwanza yalikuwa ni Lokomotiv Moscow 2 Athletic Bilbao 1 kwenye mechi iliyochezwa huko Urusi Wiki iliyopita.
HALI YA TIMU:
Baada ya kusuasua kwenye Msimu huu wa Ligi yao huko Uholanzi, Eredivisie, Ajax wamefanikiwa kushinda mechi yao ya pili mfululizo kwa kuichapa NEC Nijmegen bao 4-1 Wikiendi iliyopita.
Lakini, Ajax, wakiwa chini wa nguli wa Soka la Uholanzi, Frank De Boer, bila shaka, wanajua fika kuwa baada ya kuchapwa bao 2-0 huko kwao nafasi yao kusonga iko finyu katika mechi yao dhidi ya Man United Old Trafford.
Tangu mechi yao huko Amsterdam ArenA, Man United hawajacheza mechi yeyote kwa vile Wikiendi iliyopita kulikuwa ni mechi za FA Cup tu na wao walishatupwa nje ya michuano hiyo.
WACHEZAJI:
Staa wa Man United Wayne Rooney hatakuwepo kwa vile ni mgonjwa lakini Dimitar Berbatov huenda akacheza baada ya kupona maumivu huku kuna tetesi Kiungo chipukizi Paul Pogba huenda akapewa namba pamoja na kina Chris Smalling na Tom Cleverley.
Ajax itawakosa Nicolai Boilesen, Dmitry Bulykin na Theo Janssen lakini Beki wa zamani wa Blackburn, Andre Ooijer, anaweza kupewa namba.
REFA:
Damir Skomina ndie Mwamuzi na ndie aliechezesha mechi ambayo Napoli waliwafunga Manchester City 2-1 mapema Msimu huu kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
RATIBA:
[Matokeo Mechi za kwanza kwenye mabano]
Alhamisi Februari 23
[Saa 3 Usiku]
Athletic Bilbao v Lokomotiv Moscow [1-2]
PSV Eindhoven v Trabzonspor [2-1]
Standard Liege v Wisla Krakow [1-1]
Club Brugge v Hannover [1-2]
Valencia v Stoke City [1-0]
Twente v Steaua Bucharest [1-0]
Paok Salonika v Udinese [0-0]
Metalist Kharkiv v Red Bull Salzburg [4-0]
[Saa 5 Dak 5 Usiku]
Olympiakos v Rubin Kazan [1-0]
Manchester United v Ajax [2-0]
Atlético Madrid v Lazio [3-1]
Besiktas v Sporting Braga [2-0]
Anderlecht v AZ Alkmaar [0-1]
Sporting Lisbon v Legia Warsaw [2-2]
Schalke v Viktoria Plzen [1-1]
RAUNDI YA MTOANO TIMU 16:
Mechi kuchezwa Machi 8 na marudio Machi 15
[Timu inayotajwa kwanza ipo nyumbani]
FC Salzburg/Metalist Kharkiv v Rubin Kazan v Olympiacos
Legia Warszawa/Sporting Club v FC Porto/Manchester City
Steaua Bucuresti/FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke
AZ Alkmaar/Anderlecht v Udinese/PAOK
Stoke City/Valencia v Trabzonspor/PSV Eindhoven
Ajax Amsterdam/Manchester United v Lokomotiv Moscow/Athletic Bilbao
Steaua Bucuresti /FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke
Wisla Krakow/Standard Liege v Hannover 96/Brugge