SOKA SPESHO

NI UEFA TENA-CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI kati ya Wiki

Jumapili, 19 Februari 2012 22:10
Chapisha Toleo la kuchapisha

UEFA_ULAYAMashindano makubwa ya Klabu za Ulaya yataingia tena dimbani katikati ya Wiki hii kwa UEFA CHAMPIONZ LIGI kuchezwa Jumanne na Jumatano mechi zake zilizobaki za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na EUROPA LIGI kuchezwa mechi za marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 hapo Jumatano na Alhamisi.

Wakongwe wa Ligi Kuu England, Chelsea, wao wapo ugenini huko Italia hapo Jumanne kucheza na Napoli kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na siku hiyo hiyo kwenye michuano hiyo Magwiji wa Ulaya, Real Madrid ya Spain watakuwa ugenini huko Urusi kucheza na CSKA Moscow.

Jumatano kutakuwa na mechi mbili za UEFA CHAMPIONZ LIGI na moja ya EUROPA LIGI ambayo Manchester City watakuwa kwao Etihad kurudiana na Mabingwa watetezi FC Porto ambao Wiki iliyopita huko Ureno waliwafunga bao 2-1.

Alhamisi Februari 23 zitachezwa mechi nyingine 15 zilizobaki za EUROPA LIGI na miongoni mwake ni Magwiji Manchester United kuwa kwao Old Trafford kurudiana na Ajax Amsterdam ambayo waliichapa 2-0 Wiki iliyopita.

RATIBA:

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Jumanne Februari 21

CSKA Moscow v Real Madrid

Napoli v Chelsea

Jumatano Februari 22

Basel v Bayern Munich

Marseille v Inter Milan

EUROPA LIGI:

[Matokeo Mechi za kwanza kwenye mabano]

Jumatano Februari 22

[Saa 2 Usiku]

Manchester City v FC Porto [2-1]

Alhamisi Februari 23

[Saa 3 Usiku]

Athletic Bilbao v Lokomotiv Moscow [1-2]

PSV Eindhoven v Trabzonspor [2-1]

Standard Liege v Wisla Krakow [1-1]

Club Brugge v Hannover [1-2]

Valencia v Stoke City [1-0]

Twente v Steaua Bucharest [1-0]

Paok Salonika v Udinese [0-0]

Metalist Kharkiv v Red Bull Salzburg [4-0]

[Saa 5 Dak 5 Usiku]

Olympiakos v Rubin Kazan [1-0]

Manchester United v Ajax [2-0]

Atlético Madrid v Lazio [3-1]

Besiktas v Sporting Braga [2-0]

Anderlecht v AZ Alkmaar [0-1]

Sporting Lisbon v Legia Warsaw [2-2]

Schalke v Viktoria Plzen [1-1]

RAUNDI YA MTOANO TIMU 16:

Mechi kuchezwa Machi 8 na marudio Machi 15

[Timu inayotajwa kwanza ipo nyumbani]

FC Salzburg/Metalist Kharkiv v Rubin Kazan v Olympiacos

Legia Warszawa/Sporting Club v FC Porto/Manchester City

Steaua Bucuresti/FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke

AZ Alkmaar/Anderlecht v Udinese/PAOK

Stoke City/Valencia v Trabzonspor/PSV Eindhoven

Ajax Amsterdam/Manchester United v Lokomotiv Moscow/Athletic Bilbao

Steaua Bucuresti /FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke

Wisla Krakow/Standard Liege v Hannover 96/Brugge

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90