UWANJA: Amsterdam ArenA
TAIMU: Saa 3 Usiku Bongo Taimu
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA Cup ilianza jana kwa mechi mbili na inaendelea kesho kwa mechi nyingine 14 huku Klabu za Jiji la Manchester ambazo ndizo zipo kileleni mwa Ligi Kuu England zikicheza ugenini.
Manchester City wao wako huko Ureno kuwavaa Mabingwa watetezi wa Kombe hili FC Porto na Mabingwa wa England, Manchester United, wao wapo Amsterdam kucheza na Ajax Amsterdam kwenye Uwanja wa Amsterdam ArenA.
Timu ya tatu ya England kucheza kwenye michuano hii ni Stoke City ambao watakuwa nyumbani kucheza na Valencia ya Spain.
Mbali ya ile dhana kuwa michuano hii si mikubwa lakini ukweli ni kuwa Kombe hili si la kubeza hasa ukizichukulia Timu nzito na zenye historia huko Ulaya ambazo zimo kwenye michuano hii kama vile Ajax, Porto na Man United, ambao kati yao wameshatwaa Mataji ya Ulaya mara 14.
Man City wao walishinda Taji moja tu na hiyo ilikuwa zaidi ya Miaka 40 iliyopita pale Mwaka 1970 walipotwaa Kombe la wakati huo Kombe la Washindi.
Hata hivyo, Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, amesisitiza: ‘Silidharau Kombe hili. Bado ni Kombe la Ulaya na kuna kiwango kizuri humo. Pia hatujawahi kulitwaa!’
TAARIFA=Ajax v Man United
Ajax na Man United zimewahi kukutana mara 3 katika michuano mikubwa na mara ya mwisho ilikuwa ni kwenye Raundi ya kwanza ya Kombe la Ulaya Mwaka 1976/77 na Ajax kushinda bao 1-0 lakini kwenye mechi ya marudiano huko Old Trafford Man United walishinda bao 2-0 kwa bao za Lou Macari na Sammy McIlroy.
Ajax waliwahi kuwika Miaka ya nyuma na mara ya mwisho kutwaa Taji Ulaya ilikuwa Mwaka 1995 walipotwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini Msimu huu, ingawa ni Mabingwa watetezi, wanasuasua kwenye Ligi yao Eredivisie na wapo nafasi ya 6.
Mwaka huu Ajax wameshinda mechi moja tu na tena ni Wikiendi iliyopita walipoipiga NAC Breda 2-0 kwenye Ligi lakini wapinzani wao Man United wameshinda mechi 5 kati ya 8 zikiwemo zile za ugenini dhidi ya Man City na Arsenal
Refa:
Ni Gianluca Rocchi kutoka Italy ambae Msimu huu ameshatembeza Kadi za Njano 62 na Nyekundu 2 kwenye gemu 14 alizochezesha zikiwemo mbili za UEFA CHAMPIONZ LIGI za Arsenal, kwenye sare ya ugenini 1-1 na Borussia Dortmund, na ile ya Chelsea iliyochezwa Stamford Bridge na wao kuishinda Valencia 3-0.
Kikosi cha Man United kilichosafiri:
De Gea, Amos; Fabio, Rafael, Evans, Jones, Smalling, Fryers, Ferdinand; Valencia, Nani, Carrick, Young, Park, Scholes, Cleverley, Pogba; Rooney, Hernandez, Welbeck.
Fahamu: Giggs, Evra na Berbatov hawakusafiri
EUROPA LIGI:
Raundi ya Pili ya Mtoano:
Jumanne Februari 14
Rubin Kazan 0 Olympiacos 1
SC Braga 0 Besiktas 2
Alhamisi Februaru 16
FC Porto v Manchester City
Ajax Amsterdam v Manchester United
Lokomotiv Moscow v Athletic Bilbao
FC Salzburg v Metalist Kharkiv
Stoke City v Valencia
AZ Alkmaar v Anderlecht
Lazio v Atletico Madrid
Steaua Bucuresti v FC Twente
Viktoria Plzen v Schalke
Wisla Krakow v Standard Liege
Udinese v PAOK
Trabzonspor v PSV Eindhoven
Hannover 96 v Brugge
Legia Warszawa v Sporting Club