SOKA SPESHO

LISTI UBORA DUNIANI: Spain bado 1, Zambia ndani 50 bora, Bongo chini—ipo 139!

Jumatano, 15 Februari 2012 13:04
Chapisha Toleo la kuchapisha

FIFA-logo-300Wakati Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, bado wameendelea kushikilia nafasi ya kwanza, Mabingwa wapya wa Afrika, Zambia, wamepanda nafasi 28 na sasa wapo nafasi ya 43 katika Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo.

Tanzania imezidi kuporomoka kwa kushuka nafasi mbili na sasa ipo nafasi ya 139.

Ingawa walifungwa na Zambia kwenye Fainali ya AFCON, Ivory Coast imebaki ndiyo Timu ya juu kabisa toka Afrika na inashikilia nafasi ya 15 baada ya kupanda nafasi mbili.

Katika 10 bora, Germany imepanda nafasi moja na ipo nafasi ya pili na Argentina imetupwa nje ya 10 bora na Denmark ambao wamechukua nafasi ya 10.

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani itatolewa hapo tarehe 7 Machi 2012.

KUMI BORA:

1 Spain

2 Germany

3 Netherlands

4 Uruguay

5 England

6 Portugal

7 Brazil

8 Italy

9 Croatia

10 Denmark

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1