Kuanzia Jumanne Februari 14, Ulaya itazizima kwa ile michuano mikubwa ya UEFA ya katikati ya Wiki kwa mechi za CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI ambazo zimeingia Raundi za Mtoano na huko England Wikiendi kutakuwa na mechi za Raundi ya 5 ya FA Cup pekee bila ya zile za Ligi Kuu ambazo zitakuwa mapumzikoni hadi Wikiendi ya Februari 25.
Katika Mechi za Ulaya, kwa England, Arsenal itashuka dimbani huko San Siro, Italia kuwakwaa AC Milan katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano wa Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI hapo Jumatano Februari 15.
Wenzao toka England ambao wapo nao kwenye CHAMPIONZ LIGI ni Chelsea na wao wako ugenini lakini watacheza Jumanne Februari 21 na Napoli ya Italia.
Alhamisi Februari 16 ni Usiku wa EUROPA LIGI na safari hii huko England ipo shamrashamra kubwa kwa Kombe hili kwa vile Mabingwa wa England, Manchester United, na vinara wa Ligi, Manchester City, wamo kwenye kinyang’anyiro hiki ambacho pia wapo Stoke City.
Hapo Alhamisi Februari 16, Man United watakuwa ugenini huko Uholanzi kupambana na Ajax Amsterdam na Man City nao wako ugenini huko Ureno kucheza na FC Porto.
Stoke City wao wako nyumbani kuivaa Valencia.
RATIBA KAMILI:
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Jumanne Februari 14
Bayer Leverkusen v FC Barcelona
Lyon v Apoel Nicosia
Jumatano Februari 15
Zenit v Benfica
AC Milan v Arsenal
Jumanne Februari 21
CSKA Moscow v Real Madrid
Napoli v Chelsea
Jumatano Februari 22
Basel v Bayern Munich
Marseille v Inter Milan
EUROPA LIGI:
Jumanne Februari 14
Rubin v Olympiakos
Braga v Besiktas
Alhamisi Februari 16
Lokomotiv v Athletic Bilbao
AZ Alkmaar v Anderlecht
Ajax v Man United
Plzen v Schalke
Lazio v Athletic Madrid
Legia Warsaw v Sporting Lisbon
Salzburg v Metalist Kharki
FC Porto v Man City
Steau Bucharest v FC Twente
Hannover v Club Brugge
Stoke City v Valencia
Trabzonspor v PSV Eindhoven
Udinese v PAOK Salonika
Wisla Krakow v Sandard Liege
FA CUP:
Raundi ya 5
Jumamosi Februari 18
Millwall v Bolton
Sunderland v Arsenal
Norwich v Leicester
Chelsea v Birmingham
Everton v Blackpool
Jumamosi Februari 18
Stevenage v Tottenham
Crawley v Stoke
Liverpool v Brighton