SOKA SPESHO

Stuart Pearce kumrithi kwa muda Capello

Alhamisi, 09 Februari 2012 16:24
Chapisha Toleo la kuchapisha

STUART_PEARCEKufuatia kujiuzulu kwa Meneja wa England Fabio Capello, Mwenyekiti wa Chama cha Soka England, FA, David Bernstein, amesema Timu ya Taifa ya England itakuwa chini ya Stuart Pearce ambae ni Meneja wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana wa chini ya Miaka 21 na ambae pia alikuwa mmoja wa Wasaidizi wa Capello kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya England na Holland itakayochezwa Wembley hapo Februari 29.

Pearce ni Nahodha wa zamani wa England na aliwahi pia kuwa Meneja wa Manchester City kwa Miaka miwili kuanzia 2005.

Nafasi ya Meneja wa England ipo wazi kuanzia jana baada ya Fabio Capello kujiuzulu kufuatia mgogoro wake na FA baada ya Nahodha wa England John Terry kuondolewa kwenye wadhifa huo na FA kwa sababu ya kukabiliwa na Kesi Mahakamani ambayo itanguruma Julai 9 ya kumtukana kibaguzi Beki wa QPR Antoin Ferdinand Mwezi Oktoba katika mechi ya Ligi kati ya QPR na Chelsea.

Bernstein pia amesema wataanza zoezi la kumtafuta Meneja wa kudumu kwa uangalifu na watapendelea Meneja huyo awe Mwingereza ingawa hakufuta kabisa uwezekano wa kazi hiyo kupewa Kocha ambae si Mwingereza.

Akizungumzia nini kilijiri hata Capello akajiuzulu, Bernstein alisema wao kwenye FA walitegemea Kesi ya Terry itaendeshwa Mwezi Machi au Aprili na hivyo kumalizika kabla ya michuano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2012, itakayochezwa kuanzia Juni 8 lakini ilipopangiwa Julai 9 ikiwa Wiki moja baada ya EURO 2012 kumalizika ilibidi wachukue uamuzi wa haraka kumtoa Terry na walimjulisha hilo Capello Alhamisi Wiki iliyopita.

Bernstein alikiri Capello hakufurahishwa na uamuzi wa FA na Jumapili akaongea kwenye TV huko kwao Italia akiipinga waziwazi FA ndipo jana wakakutana na Meneja huyo na yeye mwenyewe akaamua kujiuzulu.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1