RATIBA/MATOKEO:
Robo Fainali
Jumanne Februari 7
Holstein Kiel 0 Borussia Dortmund 4
Jumatano Februari 8
TSG Hoffenheim v SpVgg Gr. Furth
Hertha Berlin v Borussia Monchengladbach
VfB Stuttgart v Bayern Munich
Taarifa:
Mabingwa watetezi na vinara wa Bundesliga Borussia Dortmund wametinga Nusu Fainali ya German Cup baada ya kuinyuka Timu ya Daraja la 4 Holstein Kiel bao 4-0 katika mechi ya Robo Fainali waliyocheza ugenini.
Kiel, ambao walileta mshangao huko Ujerumani kwa kuzitoa Timu mbili za Daraja la Kwanza na moja ya Bundesliga kabla kufika Robo Fainali, walianza vyema mechi ya jana kwa kuibana Borussia Dortmund lakini mfungaji wao bora Dortmund Robert Lewandowski aliwaua kwa kupachika bao la kwanza katika dakika ya 11.
Mchezaji wa Kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa, aliongeza bao la pili na bao nyingine kufungwa na Lucas Barrios na Ivan Perisic na hivyo kuifanya Borussia Dortmund itoke kidedea kwa bao 4-0.
Mechi nyingine 3 za Robo Fainali zitachezwa leo kwa mechi mbili za Timu za Bundesliga, VfB Stuttgart v Bayern Munich na Hertha Berlin v Borussia Monchengladbach na nyingine ni ya Timu ya Daraja la Pili Greuther Fuerth itakapocheza na ile ya Bundesliga, Hoffenheim.