SOKA SPESHO

Tarehe 6 Februari 1958==MAAFA KWA MAN UNITED!

Jumatatu, 06 Februari 2012 21:43
Chapisha Toleo la kuchapisha

MUNICH_DISASTER13Ndege ya kukodi iliyoibeba Timu ya Manchester United kutoka kwenye mechi ya Kombe la Ulaya waliyocheza na Red Star Belgrade huko Yugoslavia ilitua Uwanja wa Ndege wa Riem huko Munich, Ujerumani ili kujaza mafuta.

Wakati huo Kiwanja hicho kilikuwa kimefunikwa na theluji nyingi na mara mbili Ndege hiyo ilishindwa kuruka na ilipojaribu mara ya 3 ikatoka nje ya Barabara ya Kurukia na kwenda kugonga Nyumba mbili na kulipuka moto.

Wachezaji wanane wa Timu hiyo wenye umri mdogo wa wastani wa Miaka 24 tu walifariki na walikuwemo Nahodha Roger Byrne, Mark Jones, Eddie Colman, Tommy Taylor, Liam Whelan, David Pegg, Duncan Edwards na Geoff Bent.

Meneja wa Timu Matt Busby alipona lakini alijeruhiwa vibaya na mara mbili akiwa Hospitali aliwahi kusaliwa Sala ya mwisho.

Matt Busby, ambae baadae alipewa wadhifa na Malkia wa Uingereza na kuitwa Sir, alipopona alikijenga upya Kikosi cha Manchester United.

Kabla haijatimia Miaka mitano toka kwenye maafa hayo makubwa Manchester United ilituwa Wembley Mwaka 1963 na kutwaa FA Cup baada ya kuifunga Leicester City.

Kikosi hicho kilichotwaa Taji hilo kiliundwa na Wachezaji chipukizi kina Johnny Giles, Nobby Stiles na Bobby Charlton [pichani akiwa Hospitali mara baada ya ajali] alienusurika ajali hiyo.BOBY_CHARLTON_IN_HOSP

Kikosi hicho kikaimarika zaidi baada ya kuwepo kina George Best, Dennis Law na Bobby Charlton ambao wote hao waliwahi kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Ulaya.

Kikosi hicho kilitwaa Ubingwa wa England Mwaka 1965 na 1967 na kuwa Timu ya kwanza kabisa kwa England kuchukua Ubingwa wa Ulaya Mwaka 1968 walipoifunga Benfica iliyokuwa na Supastaa Eusebio bao 4-1 Uwanjani Wembley.

Ukipita leo mbele ya Old Trafford utakuta Sanamu za Sir Matt Busby na zile za pamoja za George Best, Dennis Law na Bobby Charlton.

Dennis Law na Bobby Charlton, ambae bado ni Mkurugenzi Klabuni, wapo bado lakini George Best alifariki na siku Jeneza lake linasindikizwa kwenda nyumbani kwao huko Ireland kutoa heshima za mwisho, Mtaani kwao liliwekwa Bango kubwa:

-Maradona Good

-Pele Better

-George BEST

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA