SOKA SPESHO

Man City, Balotelli mikono juu, kifungo Mechi 4!!

Jumatano, 25 Januari 2012 22:37
Chapisha Toleo la kuchapisha

Manchester City imeamua kutokata rufaa kupinga mashitaka dhidi ya ‘Toto Tundu’ wao Mario Balotelli aliyofunguliwa na FA baada ya kuonekana akimtimba kichwani Scott Parker wa Tottenham na hivyo atatumikia kifungo cha mechi 4 kinachoanzia mechi ya leo ya marudiano ya Nusu Fainali ya Carling dhidi ya Liverpool.

Mechi nyingine ambazo atazikosa Balotelli ni zile za Ligi Kuu England dhidi ya Everton, Fulham na Aston Villa.

Mashitaka ya Balotelli yalizuka kwa kitendo chake hicho kilichotokea kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumapili iliyopita ambayo Man City walishinda 3-2 na bao la ushindi kufungwa na Balotelli katika dakika za majeruhi kwa penati.

Kawaida makosa kama ya Balotelli ni kifungo cha mechi 3 lakini kwa vile alishawahi kutolewa kwa Kadi Nyekundu Msimu huu katika mechi na Liverpool Mwezi Novemba kifungo huwa kinakuwa mechi 4.

Wakati Balotelli anaanza kifungo chake leo, Mchezaji mwingine wa Man City aliekuwa kwenye kifungo cha mechi 4, Vincent Kompany, ambae nae alipewa Kadi Nyekundu walipofungwa na Man United kwenye FA Cup, leo ndio anamalizia mechi yake ya mwisho ya kifungo chake ambacho pia Man City walinywea kukata rufaa aliposhitakiwa na walikubali adhabu ya mechi 4 kwa vile pia aliwahi kupewa Kadi Nyekundu mwanzoni mwa Msimu huu.

Balotelli aliejiunga na Man City Mwaka 2010 tayari ameshatolewa kwa Kadi Nyekundu mara 3 na ana vituko kadhaa nje ya Uwanja kikiwemo kile cha kuunguza Nyumba aliyokuwa akiishi kwa kulipua fataki.

Maoni 

 
0 # joseph 2012-01-26 12:29
Hivi haujawahi kufanyika uchunguz kwa huyu kijana kama kweli hatumii mmea haramu!!?
Reply | Reply with quote | Quote
 

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1