RATIBA/MATOKEO:
Jumanne, Januari 24
Cardiff City 1 Crystal Palace 0 (Jumla ya Magoli 1-1, Cardiff wapita kwa penati 3-1)
Jumatano, Januari25
Liverpool v Man City (Jumla ya Magoli 1-0)
FAINALI
Jumapili Februari 26
Cardiff City v Liverpool/Man City
TAARIFA:
Kipa wa Cardiff City Tom Heaton, ambae ametokea Timu ya Vijana ya Manchester United, jana alikuwa shujaa mkubwa kwa kuokoa penati mbili na kuibeba Timu yake kwenda Wembley kwenye Fainali ya Carling Cup wakati walipopigiana mikwaju ya penati tano tano baada ya kwenda sare ya jumla ya bao 1-1 katika mechi mbili na Crystal Palace.
Crystal Palace walishinda mechi ya kwanza ya Nusu Fainali kwa bao 1-0 lililofungwa na Anthony Gardner na jana Anthony Gardner alifunga tena bao, bao la kujifunga mwenyewe katika dakika ya 7, na kuwapa ushindi Cardiff City wa bao 1-0.
Kwa vile jumla ya mabao ilikuwa 1-1 katika mechi mbili Timu hizi zilipelekwa kwenye dakika 30 za nyongeza huku Crystal Palace wakicheza Mtu 10 baada ya McCarthy kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye dakika ya 78.
Hadi dakika 120 zinamalizika mabao yalibaki 1-1 na ndipo ikaja tombola ya mikwaju ya penati ambazo Kipa Tom Heaton aliokoa mbili na Cardiff City kuishinda Crystal Palace kwa penati 3-1.
Cardiff City imetinga Fainali na inamngoja mshindi wa mechi ya leo kati ya Liverpool na Man City huku Liverpool wakiwa wameshinda bao 1-0 katika mechi ya kwanza.

![]() |