Licha ya kurudi Jijini Manchester toka likizo isiyo na ruhusa na kuripoti Klabuni Manchester City Siku 4 zilizopita, Carlos Tevez amegandishwa tu na hadi sasa hajakutana na Meneja Roberto Mancini.
Wachunguzi wanahisi kuwa hali hii imetokana na kauli ya Tevez aliyoitoa huko kwao Buenos Aires, Argentina kabla kurudi Manchester kuwa Klabu hiyo ilimtendea kama ‘mbwa’.
Valencia aliogopa kaumia sana!
Winga wa Manchester United Antonio Valencia alikumbwa na wasiwasi mkubwa alipoumia Alhamisi iliyopita kwenye mechi ya EUROPA LIGI na Ajax huko Amsterdam, Uholanzi ambayo Man United walishinda 2-0.
Hata hivyo Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson amesema Winga huyo ameumia musuli za pajani na atakuwa nje kwa muda usiozidi Wiki 4.
Lakini Valencia amesema alipokumbuka alivyovunjika enka Miezi 17 iliyopita alipatwa na wasiwasi kuwa ameumia vibaya.
Alisema: ‘Nilikuwa na wasiwasi lakini baada ya uchunguzi Madaktari wamesema ntacheza tena ndani ya Mwezi mmoja.’
Vidic huenda akarudi Uwanjani kabla Msimu kwisha
Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic anaendelea vizuri kupona goti lake alilofanyiwa upasuasi baada ya kuumia kwenye mechi na Basel ya Uswisi hapo Desemba 7 na huenda akaonekana tena Uwanjani kabla Msimu huu kumalizika.
Awali ilikuwa imekadiriwa Vidic atakua nje ya Uwanja kwa Miezi 12 lakini inaelekea ana maendeleo mazuri mno na tayari ameanza mazoezi ya kulipa nguvu goti lake la kulia alilopasuliwa.
Neill Warnock Meneja mpya Leeds United
Neil Warnock ameteuliwa Meneja mpya wa Leeds United ambayo imekuwa haina Meneja tangu Februari 1 baada ya kutimuliwa Simon Grayson.
Warnock, aliekuwa Meneja wa QPR na nae kutimuliwa Mwezi Januari baada ya Mechi 8 bila ushindi, amesaini Mkataba na Leeds mwishoni mwa Msimu wa 2012/13.