SOKA LA DUNIA

REFA LIGI KUU England ashushwa Daraja

Alhamisi, 16 Februari 2012 08:45
Chapisha Toleo la kuchapisha

REFA_ATWELLRefa Stuart Attwell, mwenye umri wa Miaka 29, ametimuliwa kuchezesha mechi za Ligi Kuu England baada ya kufanya matukio mengi ya kuboronga na kurudishwa kuchezesha mechi za Madaraja ya chini.

Attwell, akiwa na Miaka 25 Msimu wa Mwaka 2008/9, aliingizwa kwenye lile Kundi maalum la Marefa wanaochezesha mechi za Ligi Kuu na Makombe makubwa lakini Wiki chache baada ya kuanza kazi hiyo akakumbwa na skandali kubwa pale alipokubali bao la Reading wakati Mchezaji wa Watford John Eustace alikuwa tayari kautoa mpira nje kwa Mita 4 na kurudishwa tena ndani na kupachikwa bao huku Msaidizi wa Refa huyo akiashiria goli.

Goli hilo lilibatizwa jina la ‘goli la mazimwi.’

Hivi karibuni, Mwezi Desemba, Refa Stuart Attwell alimtoa nje kwa Kadi Nyekundu Beki wa Bolton, Gary Cahill [sasa yupo Chelsea] kwa kumchezea rafu Scott Parker wa Tottenham kwenye mstari wa katikati ya uwanja kwa madai Cahill alikuwa Mchezaji wa mwisho na alimzuia Parker kwenda kufunga bao.

Bolton walikata Rufaa na Kadi Nyekundu kwa Gary Cahill ilifutwa.

Mwaka 2010, kwenye mechi kati ya Liverpool na Sunderland, Liverpool walipata goli la utata mkubwa pale Sunderland walipopewa frikiki na Refa Stuart Attwell wakiwa upande wao wa uwanja na Beki wa Sunderland Michael Turner akamsogezea Kipa wake Simon Mignolet wake ili apige frikiki hiyo lakini Fernando Torres akachomoka na kufunga na Attwell akakubali bao hilo kwa madai Turner aliucheza mpira huo.

Akizungumza kuhusu kuporomoshwa Refa huyo, Refa maarufu wa zamani, Mike Riley, ambaye ndie Mkuu wa PGMOL [Professional Game Match Officials Limited], wanaosimamia Marefa wa Kulipwa, alisema wao wana wajibu mkubwa wa kuweka Marefa wenye uadilifu mkubwa hasa kwenye Ligi Kuu na Attwell atapata nafasi nyingine ikiwa ataendelea vizuri kwenye Madaraja ya chini.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA