MATOKEO:
Jumanne Februari 14
Bayer Leverkusen 1 FC Barcelona 3
Lyon 1 Apoel Nicosia 0
TAARIFA:
Bao mbili za Fowadi kutoka Chile Alexis Sanchez zimeisaidia Barcelona, Mabingwa watetezi wa Ulaya, kuishinda kwa bao 3-1 Bayer Leverkusen huko Ujerumani katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa jana usiku.
Sanchez alifunga bao la kwanza dakika ya 41 na la pili dakika ya 55.
Bayer Leverkusen walipata bao lao dakika ya 52 kupitia Michal Kadlec na kuifanya gemu iwe 1-1 wakati huo.
Bao la 3 la Barcelona lilifungwa dakika ya 88 na Lionel Messi.
Timu hizi zitarudiana hapo Machi 7.
Lyon 1 APOEL Nicosia 0
Katika mechi nyingine ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Ufaransa, Lyon iliwachapa Apoel Nicosia ya Cyprus kwa bao 1-0 kwa bao la dakika ya 58 la Alexandre Lacazette.
RATIBA:
[Mechi ni Saa 4 Dak 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Februari 15
Zenit v Benfica [Saa 2 Usiku]
AC Milan v Arsenal
Jumanne Februari 21
CSKA Moscow v Real Madrid
Napoli v Chelsea
Jumatano Februari 22
Basel v Bayern Munich
Marseille v Inter Milan