SOKA LA DUNIA

AVB kutua Chelsea ni makosa!

Jumanne, 14 Februari 2012 16:36
Chapisha Toleo la kuchapisha

ANDRE_VILLAS-BOASMwajiri wa zamani wa Andre Villas-Boas wa huko kwao Ureno wa Klabu ya FC Porto, Jorge Nuno Pinto da Costa, ametamka kuwa ni makosa kwa Meneja huyo Kijana kuhamia Chelsea.

Villas-Boas, mwenye Miaka 34, ameanza vibaya kibarua chake huko Chelsea na ameshindwa kuipeleka pale Chelsea ilipokuwa Miaka ya hivi karibuni na kwenye Ligi Kuu wako nafasi ya 5 wakiwa nje ya zile nafasi 4 za juu kwa Timu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Pia, Jorge Nuno Pinto da Costa amesema kivuli cha Mreno mwenzake, Jose Mourinho, ambae alikuwa na mafanikio makubwa katika Klabu zote mbili FC Porto na Chelsea kinamsakama Villas-Boas.

Pinto da Costa ametamka: ‘Villas-Boas ameenda Chelsea kwa sababu ya ofa kubwa ya fedha, Euro Milioni 15 lakini hilo ni kosa!’

Pinto da Costa anaamini Villas-Boas hawezi kupata mafanikio kama ya Mourinho na pia baadhi ya Wachezaji wakongwe huko Chelsea akiwataja, John Terry, Frank Lampard na Didier Drogba, ni kikwazo kwake kufanikiwa kwa vile bado ni Watu wa Mourinho hivyo ili afanikiwe inabidi aijenge Timu yake upya mwenyewe.

Hata hivyo, Pinto da Costa amekiri kuwa endapo Villas-Boas atapewa muda mrefu huko Chelsea Timu hiyo itafanikiwa.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1