SOKA LA DUNIA

McCarthy afukuzwa Wolves, Abramovich atinga mazoezini Chelsea kumhoji AVB

Jumatatu, 13 Februari 2012 16:40
Chapisha Toleo la kuchapisha

ANDRE_VILLAS-BOASWolverhampton Wanderers leo imemtimua Meneja wao Mick McCarthy kufuatia kutandikwa bao 5-1 wakiwa nyumbani na watani zao West Bromwich Albion hapo jana kwenye mechi ya Ligi Kuu England na huko Chelsea Mmiliki wake Roman Abramovich ametinga kwenye kambi ya mazoezi ya Chelsea iliyopo Cobham hapo jana Jumapili ambapo Wachezaji wote walifutiwa mapumziko yao na kutakiwa kufanya mazoezi ya ziada baada ya Jumamosi kuchapwa bao 2-0 na Everton kwenye mechi ya Ligi.

Taarifa toka Klabuni Wolves imesema uongozi umelazimika kumuondoa Mick McCarthy mara moja kufuatia mwenendo mbovu uliowafanya wapate Pointi 14 tu katika mechi zao 22 za Ligi na Msaidizi wa Meneja huyo, Terry Connor, ndie atakaimu nafasi hiyo hadi Meneja wa kudumu atakapopatikana.

McCarthy alijiunga na Wolves Julai 2006 na kuiongoza Timu kutwaa Ubingwa wa Daraja la Championship Msimu wa 2008/9 na kupanda kuingia Ligi Kuu ambako wako mpaka sasa ila Msimu huu wapo nafasi ya 3 toka mkiani.

Wakati huo huo kuvamia kwa Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, kambi ya mazoezi hapo Jumapili ambapo Wachezaji walifutiwa ofu yao na kulazimishwa kufanya mazoezi ya ziada ili kufanya mazungumzo ya dharura na Meneja Andre Villas-Boas kumeelezwa kuwa ni kitu cha kawaida na hivyo kuondoa hofu ya kung’oka kwa Meneja huyo Kijana.

Hata hivyo kuna duru za wachunguzi wanaohisi siku za Andre Villas-Boas sasa zimeanza kuhesabika.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA