SOKA LA DUNIA

Rummenigge: ‘Kipigo cha Chelsea kinauma kupita cha Man United 1999!!’

Jumapili, 20 Mei 2012 18:19
Chapisha Toleo la kuchapisha

CHELSEA_BINGWA_ULAYAMmoja wa Viongozi wakuu wa Bayern Munich ambae pia ni Nguli wa zamani wa Timu ya Taifa ya Germany na Klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge, amesema kushindwa na Chelsea jana kunauma zaidi kupita walivyobwagwa na Manchester United kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 1999 kwa bao 2-1.

Jana Jumamosi, wakiwa Uwanja wa nyumbani Allianz Arena, Bayern Munich walitoka sare bao 1-1 na Chelsea na kubwagwa kwa mikwaju ya penati 4-3.

Bayern Munich, Uwanja wa Nou Camp, Barcelona Mwaka 1999, walikuwa wakiongoza bao 1-0 hadi Dakika ya 89 na Manchester United wakasawazisha kwa bao la Teddy Sheringham na kupiga bao la pili la na la ushindi Dakika ya 92 kwa bao la Ole Gunnar Solksjaer.

Rummenigge amesema: ‘Mwaka 1999 niliumia sana kwenye Fainali ile lakini hii ya kufungwa kwetu inauma zaidi! Hatukustahili hii!’

=================

TIMU ZA ENGLAND ZILIZOWAHI KUWA BINGWA WA ULAYA:

Liverpool (Mara 5)

Manchester United (3)

Nottingham Forest (2)

Aston Villa (1)

Chelsea (1)

=================

 

Rafael achukuliwa Timu ya Taifa Brazil

Jumamosi, 19 Mei 2012 09:11
Chapisha Toleo la kuchapisha

RAFAELFulbeki wa Manchester United, Rafael, ameitwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kumbadili Daniel Alves wa Barcelona ambae aliumia majuzi mazoezini akiwa na Klabu yake.

Brazil, chini ya Kocha Mano Menezes, inatarajiwa kucheza Mechi za kirafiki baadae Mwezi huu  ikiwa ni maandalizi yao ya kushiriki Michuano ya London ya Olimpiki Mwezi Julai.

Uteuzi wa Rafael unafanya Brazil iwe na Wachezaji 18 wenye chini ya Miaka 23 ambao ndio wanaruhusiwa kucheza Olimpiki na ni watatu tu wenye zaidi ya umri huo ndio wanatakiwa wawemo kwenye Kikosi rasmi cha Wachezaji 23.

Wachezaji ambao wana umri wa zaidi ya Miaka 23 walioitwa awali Kikosini ni Kipa Jefeerson na Mabeki Thiago Silva, David Luiz, Marcelo na Daniel Alves.

Shirikisho la Soka la Btazil, CBF, limesema Kocha Menezes atakuwepo Munich, Germany kushuhudia Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya Bayern Munich na Chelsea na pia ndio Mji ambao Kikosi cha Brazil kitajumuika kwa ajili ya Mechi yao ya kirafiki na Denmark itakayochezwa Mei 26.

Kikosi kamili:

Makipa: Jefferson (Botafogo), Neto (Fiorentina), Rafael (Santos)

Mabeki: Rafael Da Silva (Manchester United), Marcelo (Real Madrid), Danilo, Alex Sandro (both Porto), Thiago Silva (AC Milan), David Luiz (Chelsea), Bruno Uvini (Tottenham Hotspur), Juan (Inter Milan)

Viungo: Casemiro, Lucas (both Sao Paulo), Sandro (Tottenham Hotspur), Romulo (Vasco da Gama), Paulo Henrique Ganso (Santos), Oscar (Internacional), Giuliano (Dnipropetrovsk)

Mafowadi: Alexandre Pato (AC Milan), Hulk (Porto), Leandro Damiao (Internacional), Neymar (Santos), Wellington Nem (Fluminense)

RATIBA MECHI ZA BRAZIL:

Mei 26=Brazil v Denmark [Mjini Hamburg, Germany]

Mei 30=USA v Brazil [Washington, USA]

Juni 3=Brazil v Mexico [Dallas, USA]

Juni 9=Brazil v Argentina [New Jersey,USA]

 

JOEY BARTON=’UKOROFI’ katika Maisha yake!

Jumatano, 16 Mei 2012 08:11
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • JOEY_BARTON• HATARINI kufungiwa Mechi 10!!!
  • • ALIWAHI kutupwa LUPANGO!!
  • • PFA yakerwa na Vituko vyake!

=======================

MIKASA YAKE:

-2004, akiwa Man City alimwunguza jichoni Mchezaji Chipukizi James Tandy

-2007, alimpiga Mchezaji mwingine Ousmane Dabo hadi akatibiwa Hospitalini

-2008 alifungwa Jela Miezi 6 kwa kushambulia na kujeruhi Mtu.

=======================

Wakati Timu yake QPR ikipigania kutoshushwa Daraja na yeye ndie Nahodha, Joey Barton alimpiga kipepsi Carlos Tevez wa Manchester City kwenye Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanja wa Etihad Jumapili iliyopita kwenye tukio ambalo mpira haukuwepo kwao na Mshika Kibendera akaona tukio hilo na kumtonya Refa Mike Dean ambae alimpa Kadi Nyekundu.

Akiwa anatoka nje ya Uwanja, Joey Barton akampiga teke Mchezaji mwingine wa Man City, Sergio Aguero na kujaribu kumpiga kichwa Vincent Kompany.

Kwa kosa la Kadi Nyekundu, Joey Barton atatumikia kifungo cha Mechi 3 lakini kwa vile alishawahi kutolewa kwa Kadi Nyekundu Msimu huu adhabu inaongezwa kuwa Mechi 4.

Matukio hayo yanayomhusu Aguero na Kompany yameifanya FA, Chama cha Soka England, kimfungulia mashitaka Joey Barton kwa vile Refa alishamwadhibu kwa Kadi Nyekundu.

PFA wanyosha mikono kwa Barton!

Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa PFA [Professional Footballers' Association], Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, Gordon Taylor ameelezea kukerwa kwa mkasa huu wa Joey Barton.

Taylor amesema: ‘Nahisi ni kama kujaribu kupandisha jabali kubwa juu ya Mlima, linateleza na kurudi chini na unakaa na kuwaza urudie tena kulipandisha? Tumejaribu kumsaidia Joey Barton na inakuwa sio rahisi. Hii ni hatua moja nyuma.’

 

SIR ALEX AWAPONGEZA MAN CITY KWA UBINGWA!

Jumapili, 13 Mei 2012 20:49
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • • ASISITIZA: ‘Tunakubali changamoto, tutarudi!’

Sir Alex Ferguson ametoa hongera kwa Mahasimu wao Manchester City kwa leo kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu baada ya kufungana Pointi na Manchester United lakini wao kubeba Kombe kwa ubora wa tofauti ya magoli.

Huu ni Ubingwa wa 3 katika historia ya Man City baada ya kuutwaa Mwaka 1936/7 na 1967/8 na leo waliutwaa katika Dakika 2 za mwisho za majeruhi baada ya kuzinduka toka bao 2-1 nyuma na QPR na kushinda bao 3-2 na hivyo kuwapiku Man United waliokuwa wameifunga Sunderland 1-0.

Endapo Manchester United wangetwaa Taji leo hili lingekuwa Taji lao la 20 katika historia yao na la 13 tangu Ligi Kuu England ianzishwe Mwaka 1992/3.

Kwa Man City hii ni mara ya kwanza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu na Timu nyingine zilizowahi kuwa Mabingwa ni Blackburn Rovers, ambao Msimu huu wameshuka Daraja, mara moja, Arsenal, mara 3, na Chelsea, mara 3.

Sir Alex Ferguson amenena: ‘Tumekuwa na wakati mzuri! Tulishawahi kutwaa Taji mara 3 Siku ya mwisho na leo bado kidogo iwe hivyo tena. Kwa niaba ya Manchester United natoa pongezi kwa jirani zetu. Ni kitu kikubwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu. Hii ni Ligi ngumu Duniani na yeyote anaeshinda anastahili hilo!’

Aliongeza: ‘Tunakubali changamoto, sisi wazuri kwa hilo na tumeshindana na wapinzani wengi kwa muda mrefu!’

 

BRAZIL: Ronaldinho atemwa, Pato arudishwa

Jumamosi, 12 Mei 2012 06:31
Chapisha Toleo la kuchapisha

BRAZIL_SOCCER_FANSStraika wa Brazil Alexandre Pato amerudishwa kwenye Kikosi cha Brazil kitakachocheza Mechi za kirafiki Mwezi Mei na Juni lakini mkongwe Ronaldinho hakuchukuliwa.

Pato hajachezea Brazil kitambo sasa kwa kuwa majeruhi.

Brazil watacheza na Denmark na USA Mwezi Mei na Juni kukutana na wapinzani wao wa jadi Argentina na pia Mexico.

Jana Kocha wa Brazil alitangaza Kikosi chake cha Wachezaji 23 ambacho idadi yake kubwa ni Wachezaji wenye umri wa chini ya Miaka 23 ikiwa ni ishara kubwa kuwa Kikosi hiki ndicho kitakuwa kiini cha kile kitakachocheza Olimpiki huko London Mwezi Julai.

Kwenye Olimpiki Timu shiriki zinatakiwa ziwe na Wachezaji watatu tu waliozidi Miaka 23.

Wachezaji ambao wana umri wa zaidi ya Miaka 23 walioitwa Kikosini ni ni Kipa Jefeerson na Mabeki Thiago Silva, David Luiz, Marcelo na Daniel Alves.

Kikosi kamili:

Makipa: Jefferson (Botafogo), Neto (Fiorentina), Rafael (Santos)

Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Marcelo (Real Madrid), Danilo, Alex Sandro (both Porto), Thiago Silva (AC Milan), David Luiz (Chelsea), Bruno Uvini (Tottenham Hotspur), Juan (Inter Milan)

Viungo: Casemiro, Lucas (both Sao Paulo), Sandro (Tottenham Hotspur), Romulo (Vasco da Gama), Paulo Henrique Ganso (Santos), Oscar (Internacional), Giuliano (Dnipropetrovsk)

Mafowadi: Alexandre Pato (AC Milan), Hulk (Porto), Leandro Damiao (Internacional), Neymar (Santos), Wellington Nem (Fluminense)

RATIBA MECHI ZA BRAZIL:

Mei 26=Brazil v Denmark [Mjini Hamburg, Germany]

Mei 30=USA v Brazil [Washington, USA]

Juni 3=Brazil v Mexico [Dallas, USA]

Juni 9=Brazil v Argentina [New Jersey,USA]

 


Page 1 of 59

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1