OLE GUNNAR SOLSKJAER=Sasa ni ‘Fergie wa Norway’
Ijumaa, 03 Februari 2012 07:17
Aliwaambia: ‘Vijana, kama kuna chochote kilichobaki kwenu basi nitachukua pesa zenu zote, mikopo ya nyumba zenu na kuzichezea kamari kwamba tutachukua Ubingwa wa Ligi Msimu huu! Nadhani hili litatupa nafasi kubwa kushinda hiyo kamari!’ Solskjaer aliyajua maneno yote ya hotuba hiyo moyoni kwani aliyasikia zamani. Aliikariri hotuba hiyo yote Miaka 15 nyuma katika Msimu wake wa kwanza kama Mchezaji wa Manchester United pale Sir Alex Ferguson alipotoa spichi hiyo hiyo kwa Wachezaji wake wote kufuatia vipondo viwili mfululizo vya bao 5-0 toka kwa Newcastle na 6-3 toka kwa Southampton kwenye mechi za Ligi. ‘Naikumbuka Siku hiyo waziwazi!’ Solskjaer alisema huku akitabasamu. ‘Na kweli Msimu huo Man United walichukua Ubingwa kilaini!’ Na ndivyo walivyofanya Molde, chini ya Ole Gunnar Solskjaer alietua hapo Januari 2011, kwa kutwaa Ubingwa wao wa kwanza Nchini Norway tangu Klabu hiyo ianzishwe Miaka Miaka 100 iliyopita. Ole Gunnar Solskjaer alianza kujiandaa kuwa Meneja tangu akiwa mdogo na kukazania zaidi akiwa Mchezaji. Akiwa na Miaka 10 tu alikuwa akiwafundisha Watoto wenzake kucheza Soka Mtaani kwao huko Kristiansund, Norway. Akiwa Man United alikuwa akiweka Kitabu cha Kumbukumbu yote yaliyokuwa yakitokea kwenye mazoezi, mechi na hata pale Nahodha Roy Keane akitukana au akimtukana wakati akikosa goli. Lakini mwishowe Kitabu hicho cha Kumbukumbu kiligeuka kuwa kwa yale tu Sir Alex Ferguson aliyokuwa akiongea hasa mbinu, mikakati na tathmini ya Soka. Solskjaer amebaini alipotua Molde aliigeuza Klabu hiyo kama Man United ndogo kutokana na ujuzi wake wa Miaka 15 wakati akiwa Manchester kwa kuiga kila kitu kuanzia mlo wa Wachezaji, uvaaji, na mazingira mengine yote aliyojifunza akiwa Old Trafford. Alipostaafu kama Mchezaji wa Man United baada ya kuumia goti Solskjaer alipewa nafasi ya kuwa Meneja wa Timu ya Rizevu ya Man United na alipoamua kwenda Molde Solskjaer aliwachukua Makocha wasaidizi wa Man United, Mark Dempsey na Richard Hartis, ili kumpa sapoti. Inadaiwa Ole Gunnar Solskjaer, ambae yupo kwenye historia iliyotukuka ya Man United kwa kuifungia bao la ushindi dakika za majeruhi kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 1999 walipowafunga Bayern Munich bao 2-1, yupo kwenye maandalizi kurudi Old Trafford kumrithi Sir Alex Ferguson akiamua kustaafu. Kutoa maoni
|
|
|
|
|
|
|