Ligi Kuu England

DABI ya Manchester yabadilishwa Ratiba!

Jumatano, 22 Februari 2012 17:32
Chapisha Toleo la kuchapisha

MAN_UNITED_TITLE_19Mechi 5 za Ligi za Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester United, zilizokuwa zichezwe Mwezi Aprili zimepanguliwa na kupangiwa Ratiba upya ikiwemo ile Dabi kati ya Manchester City na Man United itakayochezwa Uwanja wa Etihad ili kukidhi matakwa ya Stesheni za TV ili kurusha mechi hizo laivu.

Dabi hiyo ya Manchester, ambayo awali ilikuwa ichezwe Aprili 28, sasa itachezwa Jumatatu Aprili 30 kuanzia Saa 4 Usiku, Bongo Taimu.

Mechi nyingine za Mabingwa hao zilizokumbwa na panga pangua hiyo ni pamoja na mechi za nyumbani dhidi ya QPR, Aston Villa na Everton.

Mechi nyingine iliyobadilishwa ni ile ya ugenini na Wigan.

Pia, mechi ya Man United Uwanjani Old Trafford hapo Jumamosi Machi 10 dhidi ya West Brom huenda ikabadilika ikiwa Man United watafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EUROPA LIGI.

RATIBA Iliyobadilika kwa Aprili ni:

Jumapili Aprili 8

Man United v QPR [Saa 9 na Nusu Mchana]

Jumatano Aprili 11

Wigan v Man United [Saa 3 Dak 45 Usiku]

Jumapili Aprili 15

Man United v Aston Villa [Saa 12 Jioni]

Jumapili Aprili 22

Man United v Everton [Saa 8 na Nusu mchana]

Jumatatu Aprili 30

Man City v Man United [Saa 4 Usiku]

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90