Ligi Kuu England

John Terry nje Miezi 2!

Jumanne, 21 Februari 2012 19:52
Chapisha Toleo la kuchapisha

Terry++Kuikosa mechi ya England v Holland, kutokutana na Rio England!

John Terry anatarajiwa kupasuliwa goti na hivyo kumweka nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa Miezi miwili.

Nahodha huyo wa Chelsea sasa atalikosa pambano dhidi ya Napoli litakalochezwa Jumanne usiku na pia kuchukuliwa kwenye Kikosi cha England ambacho kitacheza mechi ya kirafiki na Holland Wiki ijayo.

Terry aliumia goti lake walipoifunga Portsmouth Mwezi uliopita kwenye FA Cup na amezikosa mechi 4 za Chelsea, ambazo zote hawakushinda, lakini alitegemewa kucheza mechi na Napoli.

Hata hivyo, Terry alifanya mazoezi na wenzake jana lakini leo akalalamika ana maumivu kwenye goti ambalo limejaa maji.

Lakini kukosekana kwa Terry kuichezea England kunampunguzia kazi ngumu Kocha wa Muda Stuart Pearce ambae wengi wanahisi alikuwa na uamuzi mgumu wa kumchagua Terry na Rio Ferdinand pamoja baada ya Terry kuvuliwa Unahodha wa England kufuatia kukumbwa na tuhuma za kumtukana kibaguzi Mdogo wake Rio, Antoin Ferdinand, kwenye mechi kati ya Chelsea na QPR, na tuhuma hizo kumfikisha Terry Mahakamani ambako inategemewa kesi yake kuanza Mwezi Julai.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1