Ligi Kuu England

Torres ‘kupigwa shoka’ mechi na Napoli

Jumatatu, 20 Februari 2012 18:20
Chapisha Toleo la kuchapisha

TORRES12Fernando Torres, ambae ameigharimu Chelsea Pauni Milioni 50 Januari Mwaka jana na tangu wakati huo amefunga bao 3 tu za Ligi, huenda asicheze kabisa katika mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Chelsea itacheza ugenini Jumanne huko Italia na Napoli katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano.

Majuzi Jumamosi, Torres alianza kwenye mechi ya FA Cup walipocheza na Birmigham Uwanjani Stamford Bridge na kutoka sare bao 1-1 lakini Torres alitolewa wakati wa haftaimu wakati wapo nyuma kwa bao 1-0 na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Drogba na hatimaye Chelsea kusawazisha kwa bao la dakika ya 62 la Daniel Sturridge.

Ingawa Kocha wa Chelsea, Andre Villas-Boas, ambae nae yuko kwenye presha kubwa kwa kuboronga kwa Klabu yake Msimu huu, hajasema moja kwa moja Straika gani atacheza na Napoli lakini kidole kipo kwa Drogba ambae alipachika bao mara ya mwisho alipovaa Jezi ya Chelsea walipocheza na Aston Villa hapo Desemba 31 kabla kujiunga na Nchi yake Ivory Coast kwenye AFCON 2012 ambako aliifungia bao 3.

Mara ya mwisho kwa Torres kufunga bao ni Oktoba 19 alipoipatia Chelsea bao 2 walipoifunga Genk 5-0 kwenye mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Kabla kujiunga na Chelsea Torres alikuwa Liverpool ambako alicheza mechi 102 na kufunga bao 65.

Kabla kujiunga na Chelsea Torres alikuwa Liverpool ambako alicheza mechi 102 na kufunga bao 65.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1