MATOKEO:
Jumamosi Februari 18
Chelsea 1 Birmingham 1 [Kurudiana huko St Andrew Stadium. Tarehe kupangwa]
Millwall 0 Bolton 2
Norwich 1 Leicester 2
Everton 2 Blackpool 0
Sunderland 2 Arsenal 0
TAARIFA:
Jumatano walinyukwa 4-0 na AC Milan na kuwekwa mguu mmoja nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na leo wametandikwa 2-0 na Sunderland na kutupwa nje ya FA Cup na sasa inaelekea wazi ule ukame wa Miaka 7 wa kukosa Taji lolote utaendelea maana hata kwenye Ligi Kuu England wako nafasi ya 4 na Pointi 17 nyuma ya vinara.
Bao za Sunderland leo zilifungwa na Kieran Richardson, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, dakika ya 40 na Oxlade-Chamberlain kwa kujifunga mwenyewe mpira uliogonga posti na kurudi katika dakika ya 77.
RATIBA:
Jumapili Februari 19
[Saa 9 Mchana]
Crawley v Stoke
[Saa 11 Jioni]
Stevenage v Tottenham
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Liverpool v Brighton