Ligi Kuu England

Wenger aomba radhi kipondo Milan, RVP ashauriwa kuhama Arsenal!

Jumamosi, 18 Februari 2012 14:09
Chapisha Toleo la kuchapisha

WENGER-SITABWAGA_MANYANGAWakati Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akiomba radhi kwa Mashabiki wa Arsenal kufuatia kipigo chao cha mabao 4-0 huko Milan Jumatano iliyopita mikononi mwa AC Milan katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Straika wa AC Milan Zlatan Ibrahimovich amemshauri Nahodha wa Arsenal Robin van Persie kuhama Klabu hiyo ikiwa anataka kushinda Mataji.

Arsene Wenger, akiongea na Maripota hapo jana kabla ya safari ya Arsenal kwenda Stadium of Light kucheza na Sunderland Jumamosi katika mechi ya Raundi ya 5 ya FA Cup, amesema Mashabiki wao wamekuwa imara kwao na yeye hana budi kuomba radhi kwa matokeo mabovu.

Aliongeza: ‘Kesho ni siku nyingine na ni pambano jingine na tunataka watushangilie. Unaweza ukatoa zaidi ya sababu mia za kufungwa lakini ukweli ni kuwa tulicheza vibaya na haikuwa siku yetu!’

Sasa ni Miaka 7 tangu Arsenal watwae Taji na huku wakiwa mguu mmoja nje kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na wapo nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 17 nyuma ya vinara Manchester City, FA Cup ndio imebaki njia kubwa kwao kutwaa Taji Msimu huu.

Wenger ametamka: ‘Kombe hili ni muhimu lakini kwa vile tulivunjwa moyo mechi iliyopita FA Cup imekuwa muhimu mno!’

RVP ashauriwa kuhama Arsenal

Robin van Persie ameshauriwa kuondoka Arsenal na Straika wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic ambae ndie aliekuwa mwiba mkubwa baada ya Timu yake kuichapa Arsenal bao 4-0 Jumatano iliyopita.

Ibrahimovich ametamka: ‘Soka ni ushindi. Kama hushindi unataka kuondoka.’

Ibrahimovich aliongeza: ‘Nimeshinda Ubingwa mara 8 katika Miaka minane nikiwa na Klabu tofauti katika Nchi tofauti. Ukibweteke sehemu moja unajiona uko nyumbani na kila kitu rahisi tu. Ukihamia kwingine ni mtihani mkubwa. Ukishinda huko ndio unakuwa Bingwa wa kweli, na unaheshimika sana!’

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA