Ligi Kuu England

Ryan Giggs kuporomosha rekodi mpya, Mechi 900!!!

Jumatatu, 13 Februari 2012 17:44
Chapisha Toleo la kuchapisha

GIGGS12REKODI YAKE MAN UNITED:

Mechi: 899

Magoli: 162

Alianza kucheza: 2 Machi 1991

+++++++++++++++++++

Baada ya dakika 35 Uwanjani Old Trafford hapo Machi 2, Mwaka 1991 nguli Denis Irwin alitolewa akichechemea kwenye mechi na Everton na Meneja wa Manchester United Alex Ferguson akamwingiza Kijana wa Miaka 17 mwenye mwili mwembamba na huo ndio ukawa mwanzo wa historia ya Ryan Giggs kuichezea Klabu moja tu kwa Miaka 21.

Hadi leo Giggs ndie Mchezaji pekee katika historia ya Soka la Uingereza kutwaa Vikombe vingi na hadi leo ameshaichezea Klabu yake Man United mechi 899.

Denis Irwin anasema: ‘Inashangaza! Kabla hajaanza kucheza Timu ya kwanza tulijua ni mwepesi kama umeme wa radi, kama upepo na mwenye uwezo na kipaji kikubwa!’

Irwin, ambae alikuwa Fulbeki wa kushoto na aliechezea Man United Mechi 529, aliongeza kuwa Giggs alikuwa akicheza mbele yake kama Winga wa kushoto kwa Miaka 10 lakini mpaka leo yuko fiti na bado mwenye uwezo mkubwa.

Leo hii Giggs ana Miaka 38, amecheza Mechi 899 na Wiki hii huenda akaweka rekodi mpya ya kucheza Mechi 900 kwa Man United.

Giiggs huenda akacheza Mechi zaidi ya 900 na kuweka rekodi nyingine mpya kwani ameongeza tena Mkataba wake na Man United kwa Mwaka mmoja zaidi

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90