Ligi Kuu England

LIGI KUU England: Tathmini mechi za leo

Jumamosi, 11 Februari 2012 13:02
Chapisha Toleo la kuchapisha

MAN_UNITED_v_LIVERPOOL-11FEB12RATIBA:

Jumamosi Februari 11

Saa 9 Dak 45 Mchana

Manchester United v Liverpool

Saa 12 Jioni

Bolton Wanderers v Wigan Athletic

Sunderland v Arsenal

Blackburn Rovers v QPR

Swansea City v Norwich City

Everton v Chelsea

Fulham v Stoke City

Saa 2 na Nusu Usiku

Tottenham v Newcastle United

Taarifa:

Manchester United v Liverpool

Siku zote hii ni mechi kubwa inayovutia wengi kila kona ya Dunia na leo ipo Uwanjani Old Trafford.

Hali za Vikosi:

Kiungo mahiri, chipukizi Tom Cleverly, atakuwemo kwenye Kikosi cha Man United baada ya kupona maumivu ya enka yaliyomweka nje kwa Miezi mitatu.

Lakini Man United watamkosa Beki Phil Jones ambae ni majeruhi ingawa mwenzake Chris Smalling amepona na huenda akachezeshwa.

Straika wa Liverpool Luis Suarez huenda akaanza mechi yake ya kwanza tangu atoke kifungo cha mechi 8 kwa kumkashifu kibaguzi Beki wa Man United Patrci Evra na leo watakutana uso kwa uso na huenda leo wakapeana mikono kabla mechi kuanza wakati Timu zinaposalimiana.

Uso kwa Uso:

Katika mechi 7 za mwisho kuchezwa Old Trafford kati ya Timu hizi, Man United wameshinda mechi 6 na Liverpool mara moja tu hiyo ikiwa ni Machi 2009.

Everton v Chelsea

Hii mechi inachezwa Uwanja wa Goodison Park kuanzia Saa 12 Jioni mara baada ya Man United kuivaa Liverpool.

Hali za Vikosi:

Mfungaji mahiri wa Everton Tim Cahill huenda akacheza baada ya kupona maumivu yake na pia Mchezaji mpya Nkica Jelavic huenda akaichezea Everton mechi yake ya kwanza Uwanjani Goodison Park.

Everton itawakosa Phil Jagielka, Leon Osman, Jack Rodwell na Seamus Coleman ambao ni majeruhi.

Chelsea huenda wakawa na Viungo Frank Lampard na John Obi Mikel baada ya kupona maumivu yao na Ashley Cole atarudi baada ya kutumikia kifungo cha mechi moja.

Uso kwa Uso:

Katika mechi mbili za mwisho kwa Chelsea kucheza Goodison Park wamefungwa mechi zote.

Sunderland v Arsenal

Hali za Vikosi:

Wachezaji wapya wa Sunderland, Wayne Bridge na Sotirios Kyrgiakos, ambao wapo hapo kwa mkopo wanaweza kucheza mechi yao ya kwanza.

Nicklas Bendtner, ambae yupo kwa mkopo Sunderland kutoka Arsenal, leo haruhusiwi kucheza kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu zinazokataza Mchezaji alie kwa mkopo kucheza dhidi ya Klabu yake iliyomwajiri.

Fulbeki wa Arsenal, Kieran Gibbs, huenda akaonekana leo baada ya kupona nyonga iliyokuwa imemuweka nje tangu mwanzoni mwa Oktoba.

Uso kwa Uso:

Arsenal hawajafungwa na Sunderland katika mechi zao 4 za mwisho walizocheza Stadium of Light lakini kati ya hizo 3 zilikuwa ni sare.

Tottenham v Newcastle United

Hali za Vikosi:

Tottenham itawakaribisha tena Jermain Defoe na Aaron Lennon waliopona maumivu yao lakini itawakosa majeruhi Ledley King, Younes Kaboul, Rafael van der Vaart na Sandro.

Baada ya kuikosa mechi iliyopita Tottenham waliposafiri kwenda kucheza na Liverpool kufuatia Ndege yake kufutiwa safari kwa ajili ya hali ya hewa mbaya, Meneja wa Tottenham Harry Redknapp leo atakuwepo Uwanjani White Hart Lane.

Uso kwa Uso:

Newcastle wamewafunga Tottenham 3-2 Msimu wa 2006/7 na 4-1 Msimu uliofuatia lakini baada ya hapo wamefungwa mechi mbili mfululizo hapo White Hart Lane.

MECHI ZIJAZO:

Jumapili Februari 12

Saa 10 na Nusu Jioni

Wolves v West Bromwich

Saa 1 Usiku

Aston Villa v Man City

[Timu zimecheza Mechi 24]

1 Man City Pointi Pointi 57

2 Man United 55

3 Tottenham 50

4 Chelsea 43

-----------------------------------

5 Newcastle 42

6 Arsenal 40

7 Liverpool 39

8 Sunderland 33

9 Norwich 32

10 Swansea 30

11 Everton 30

12 Stoke City 30

13 Aston Villa 28

14 Fulham 27

15 WBA 26

16 QPR 21

17 Wolves 21

--------------------------------

18 Bolton 20

19 Blackburn 18

20 Wigan 15

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA