Ligi Kuu England

MIMACHO Old Trafford Jumamosi==Man United v Liverpool!

Alhamisi, 09 Februari 2012 20:49
Chapisha Toleo la kuchapisha

MAN_UNITED_v_LIVERPOOL-11FEB12RATIBA:

Jumamosi Februari 11

Saa 9 Dak 45 Mchana

Manchester United v Liverpool

Saa 12 Jioni

Bolton Wanderers v Wigan Athletic

Sunderland v Arsenal

Blackburn Rovers v QPR

Swansea City v Norwich City

Everton v Chelsea

Fulham v Stoke City

Saa 2 na Nusu Usiku

Tottenham v Newcastle United

TAARIFA:

Bila shaka Wikiendi hii mimacho ya Wadau wengi wa Soka itakuwa Old Trafford kushuhudia Mabingwa Manchester United wakiwakwaa Mahasimu wao wa enzi na enzi Liverpool huku vivutio vikubwa kwenye mechi hii vikiwa kwanza hii ni BIGI MECHI, pili ushindi kwa Man United utawafanya watwae uongozi wa Ligi kwa vile vinara Man City wanacheza Siku inayofuata na tatu hii itakuwa mara ya kwanza kwa Patrice Evra kukutana na Luis Suarez tangu Straika huyo wa Liverpool kutoka kifungo cha Mechi 8 kwa kumkashifu kibaguzi Evra kwenye mechi ya Ligi iliyochezwa huko Anfield mapema Msimu huu.

++++++++++++++++++

MSIMAMO Timu za juu:

[Timu zimecheza Mechi 24]

1 Man City Pointi Pointi 57

2 Man United 55

3 Tottenham 50

4 Chelsea 43

-----------------------------------

5 Newcastle 42

6 Arsenal 40

7 Liverpool 39

++++++++++++++++++

Mbali ya hayo, hii ni mechi muhimu kwa Liverpool ambao wapo nafasi ya 7 na wako pointi 4 nyuma ya Chelsea waliokamata nafasi lulu ya 4 katika msimamo wa Ligi ikiwa ndiyo nafasi ya mwisho kwa Timu kupata fursa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Juu ya Liverpool wapo Arsenal walio pointi moja mbele yao na Newcastle ambao wako pointi mbili mbele ya Arsenal.

Kwa Man United, mbali ya kutaka kuing’oa kileleni Man City, wao pia wanataka kulipa kisasi kwa kufungwa bao 2-1 na Liverpool huko Anfield hivi karibuni na kutolewa kwenye FA Cup mechi ambayo wenyewe wanaamini fika hawakustahili kufungwa kwa jinsi walivyoitawala.

RATIBA MECHI ZIJAZO:

Jumapili Februari 12

Saa 10 na Nusu Jioni

Wolves v West Bromwich

Saa 1 Usiku

Aston Villa v Man City

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA