Mara baada ya leo Mahakama kutoa hukumu kuwa hana kosa lolote katika mashitaka yaliyomkabili ya kukwepa kulipa Kodi, Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amekiri kuwa kipindi chote cha Miaka mitano iliyopita alipokumbwa na tuhuma hizo kilikuwa ni kama Jinamizi baya kwake.
Baada ya Wazee wa Baraza la Mahakama kukaa Siku mbili wakitafakari Kesi iliyomkabili Redknapp na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Portsmouth, Milan Mandaric, Wazee hao walitoa kauli moja ya uamuzi kuwa wote wawili walikuwa hawana hatia yeyote kwenye mashitaka yao.
Mara baada ya kutoka Mahakamani baada ya kwisha Kesi hiyo iliyowagharimu Polisi Pauni Milioni 8 kuchunguza tuhuma za kuwa Mandaric alimwingizia Redknapp Pauni 189,000 kwenye Akaunti ya siri iliyobatizwa jina la Mbwa wa Redknapp Rosie huko Monaco ili kukwepa kulipa Kodi England, Redknapp amesisitiza Kesi hiyo haikupaswa kwenda Mahakamani.
Redknapp amesema: Ni Jinamizi. Ni Miaka mitano na Kesi hii haikupaswa kufika Mahakamani.’
Pia, Redknapp aliwashukuru Mawakili wake, Klabu na Mashabiki wa Tottenham pamoja na Familia yake kwa kumpa sapoti kubwa.
Maoni