Ligi Kuu England

Liverpool 0 Tottenham 0, Suarez chupuchupu!

Jumanne, 07 Februari 2012 10:04
Chapisha Toleo la kuchapisha

anfieldLiverpool jana walishindwa kuwang’oa Arsenal kutoka nafasi ya 6 baada ya kwenda sare 0-0 na Tottenham katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa huko Anfield Jijini Liverpool.

Kwenye mechi hiyo, Straika wa Liverpool kutoka Uruguay, Luis Suarez, aliingizwa Kipindi cha Pili hiyo ikiwa mechi yake ya kwanza baada ya kumaliza kifungo chake cha mechi 8 alichopewa na FA kwa kumkashifu kibaguzi Beki wa Manchester United Patrice Evra lakini aliponea chupuchupu kukumbwa na balaa jingine dakika 3 tu baada ya kuingizwa alipomtimba tumboni Kiungo wa Tottenham Scott Parker na kupewa Kadi ya Njano badala ya Kadi Nyekundu ambayo wengi walitegemea.

Bosi wa Spurs, Harry Redknapp, ambae kwa Wiki mbili sasa amekuwa akishinda Mahakamani huko London kujitetea kwenye Kesi inayomkabili ya kukwepa kulipa kodi, hakuwepo Uwanjani baada ya kushindwa kusafiri kutoka London kufuatia Ndege yake aliyopangwa kusafiria kufutwa kutokana na ukungu mzito.

Vikosi:

Liverpool: Reina, Kelly, Skrtel, Agger, Johnson, Adam, Spearing, Kuyt, Gerrard, Bellamy, Carroll

Akiba: Doni, Aurelio, Suárez, Henderson, Coates, Downing, Carragher.
Tottenham: Friedel, Walker, Dawson, King, Assou-Ekotto, Parker, Livermore, Kranjcar, Modric, Bale, Adebayor

Akiba: Cudicini, Saha, Rose, Nelsen, Khumalo, Luongo, Lancaster.
Refa: Michael Oliver .

RATIBA MECHI ZIJAZO:

Februari 11

Saa 9 Dak 45 Mchana

Manchester United v Liverpool

Saa 12 Jioni

Bolton Wanderers v Wigan Athletic

Sunderland v Arsenal

Blackburn Rovers v QPR

Swansea City v Norwich City

Everton v Chelsea

Fulham v Stoke City

Saa 2 na Nusu Usiku

Tottenham v Newcastle United

Februari 12

Saa 10 na Nusu Jioni

Wolves v West Bromwich

Saa 1 Usiku

Aston Villa v Man City

MSIMAMO:

[Timu zimecheza Mechi 24]

1 Man City Pointi Pointi 57

2 Man United 55

3 Tottenham 50

4 Chelsea 43

-----------------------------------

5 Newcastle 42

6 Arsenal 40

7 Liverpool 39

8 Sunderland 33

9 Norwich 32

10 Swansea 30

11 Everton 30

12 Stoke City 30

13 Aston Villa 28

14 Fulham 27

15 WBA 26

16 QPR 21

17 Wolves 21

--------------------------------

18 Bolton 20

19 Blackburn 18

20 Wigan 15

=========

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90